fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps instagram Intaneti Maujanja Mtandao wa Kijamii

Jinsi ya kutumia Instagram Kukuza Biashara yako

Jinsi ya kutumia Instagram Kukuza Biashara yako

Spread the love

Je umewahi kujiuliza ni jinsi gani unaweza kutumia Instagram kukuza biashara yako? Kama Ndio basi makala hii itakuelezea namna ambavyo utaweza kufanya hivyo na kufanikiwa katika biashara zako kwa kufanya mauzo mtandaoni na dukani kwako pia.

Instagram ni mtandao wa kijamii unaojihusisha na utumaji wa picha na video mtandaoni na kuziweka wazi kwa mtu yeyote aliyeko hewani muda huo kuweza kuona. Mtandao huu wa kijamii ulinunuliwa na facebook na sasa hufanya kazi kwa pamoja na unaweza kuunganisha akaunti yako ya facebook na akaunti yako ya Instagram.

SOMA PIA  Tahadhari: Password meters si za kuaminika kwa asilimia zote

Instagram ina watumiaji Bilioni 1 walio hewani mtandaoni ndani ya mwezi mmoja na kutokana na idadi hii kubwa ya watumiaji imewezesha wafanya biashara wengi kuanza kutuma matangazo yao huku ili kuvutia wateja wapya katika biashara zao pamoja na kujenga mahusiano mazuri na wateja wao wa kudumu.

Ili uweze kutumia vizuri Instagram kwaajili ya biashara zako ni lazima uwe na akaunti ya kawaida kwanza ambapo utalazimika kuibadilisha akaunti hiyo kuwa akaunti ya kibiashara.

kutumia Instagram Kukuza Biashara

Ukiwa na akaunti ya biashara ya instagram unaweza kufanya mambo yafuatayo:

  • Kutengeneza duka kwenye akaunti yako; Ukiwa na akaunti ya biashara ya Instagram utakuwa na uwezo wa kutengeneza mfano wa duka lako kwa kuweka picha pamoja na taarifa muhimu za bidhaa zako kama jina, bei ya bidhaa na ukubwa uliopo au rangi zilizopo.
  • Kutuma matangazo ya kulipia yaliyowalenga wateja wako; Ukiwa na akaunti ya biashara ya Instagram utaweza kuchagua ni watu gani ungependa waone tangazo lako na pia ni maeneo gani ungependa tangazo lako lionekane sana. Kwa kufanya hivi utakuwa unajiongezea uwezekano wa wateja wapya kukutafuta na kukupata pale wanapotaka kununua bidhaa kutoka kwako.
  • Kujenga mahusiano na wateja wako; Kwa kutumia Instagram utaweza kujenge mahusiano mazuri na wateja wako wapya na wa kudumu ambapo utakuwa na uwezo wa kuwauliza maswali, kuwapigisha kura au kuweka saa inayoonyesha muda uliobaki wa ofa zako kuisha kupitia Instagram stories.

Ifahamike kuwa ili ufanikiwe vizuri katika kutumia Instagram kukuza biashara yako ni lazima uwe na mpango mkakati wa muda mrefu angalau mwezi mmoja wa mambo ambayo utakuwa ukiyachapisha kwenye akaunti yako ukiachana na bidhaa zako ili uweze kujenga mahusiano mazuri na wateja wako. Unaweza pia kusoma makala zetu zingine zinazoelezea biashara mtandaoni hapa.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania