fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
instagram Intaneti

Machi 19 Pope Francis Atajiunga na Instagram, Ingia Kujua Zaidi!

Machi 19 Pope Francis Atajiunga na Instagram, Ingia Kujua Zaidi!

Spread the love

Kwa sasa Pope Francis amejiweka tofauti na ma Pope wengine waliopita juu ya vitu vingi sana. Kwa mfano katoa sauti yake juu ya mambo mengi sana kama ndoa za jinsia moja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Pope Francis pia inasemekana kuwa anataka kuweka rekodi ya kuwa Pope ambaye anapenda teknolojia kwa kuongezea katika akaunti yake ya Twitter amesema kuwa ataweza kuingia kwa mara ya kwanza katika mtandao wa kijamii unaohusisha picha na video yaani Instagram.

Pop Francis Akiwa Na Tim Cook Wa Apple Inc.

Pop Francis Akiwa Na Tim Cook Wa Apple Inc.

Kutokana na ripoti zilizopo ni kwamba akaunti hiyo itafunguliwa ifikapo machi 19 mwaka huu. Ripoti inaongezea  kuwa Pope Francis atatumia jina la @Franciscus katika mtandao huo wa Instagram.

Pope Francis ambaye kwa kipindi cha mda mrefu amekuwa akisifu uwezo wa intaneti katika kukuza na kujenga jamii bora ambayo iko radhi ku’share’ mambo mbalimbali baina ya watu wake, amekuwa katika makutano ya siri na  bwana Kevin Systrom, ambaye ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Instagram mwezi uliopita.

Hakuna ushahidi ambao unainyesha kuwa Bw. Kevin Systrom alimwalika Pope ilimradi tuu kutengeneza akaunti yake ya instagram. Lakini kutoka kwa akaunti ya Kevin ndani ya Instagram, waliongelea juu ya jinsi gani picha inaweza ikawa na uwezo mkubwa katika kuwaleta watu karibu duniani kote bila ya kujali mipaka kama vile lugha na tamaduni.

SOMA PIA  Kuchati Facebook Kwenye Simu au Tableti Kutaitaji Messenger

Ukiachana na utakatifu wake mwingi alionao bado Pope ana Followers Milioni 8.88 katika mtandao wake wa Twitter ambapo anatumia jina la @Pontifex ambapo alijiunga mwaka 2012. Na hapo bado ana akaunti zingine 8 ambazo ni ‘Official’ na zinatumia lugha tofauti tofauti zikijumuisha kitaliano, kifaransa na kiarabu.

SOMA PIA  Soma Meseji Za WhatsApp Kwa Siri, Bila Ya Tiki Za Bluu Kuonekana!

Pope licha ya upendo wake katika Teknolojia pia ameshauri kuwa watu wasiwe wanatumia vifaa vyao wakati wa kula chakula. Na pia familia ambazo haziongei na kula pamoja ( katika Meza moja) hazihesabiki kama ni familia.

Kwa hamu kabisa, naisubiria akaunti hii ya @Franciscus katika mtandao wa Instagram. Jambo nnalolisubiria ni kuona picha ya kwanza ya pope katika akaunti hiyo na ndani ya siku moja itakuwa na followers wangapi – Kaa na mimi mkao wa kula – Zaidi tembelea TeknoKona kila siku. TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania