fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mtandao Tovuti

Jay Z Atoa Albamu Za ‘The Blueprint’ Katika Mitandao Mingine Isipokuwa Tidal!

Jay Z Atoa Albamu Za ‘The Blueprint’ Katika Mitandao Mingine Isipokuwa Tidal!

Spread the love

Jay Z licha ya kumiliki mtandao wa muziki na video, Tidal bado anahakikisha kazi zake nyingi za zamani zinaingiza pesa nyingi kwa kutumia mtandao wake huo.

Kwangu mimi inaingia akilini kabisa, kwa nini uwafaidishe wengine (wapinzani) kwa kitu ambacho unaweza kukifanya mwenyewe na kikakuingizia pato. Basi msaani huyo ameamua kutoa albamu zake zote zile za mwendelezo wa ‘Blueprint’ katika mitandao mingine inayofanya kazi kama Tidal (streaming). Hii inamaanisha kuwa katoa albumu hiyo katika mitandao mingine na kaiacha katika mtandao wake tuu yaani Tidal.

Jay Z

Jay Z

Licha ya hiyo bado albumu hiyo imejiunga na zingine za Kanye West, The Life of Pablo na singo ya Beyoncé, Formation ambazo zinapatikana katika mtandao wa Tidal tuu.

Msemaji wa mtandao wa Spotify ameweka wazi kuwa albumu za Blueprint za msanii huyo ni kweli zimeondolewa katika mtandao huu na katika mitandao mingine na miezi kadhaa imepita mpaka sasa.

Kava Ya Albamu Ya 'Blueprint' Ya Jay Z

Kava Ya Albamu Ya ‘Blueprint’ Ya Jay Z

“Tuna imani kuwa atarudisha albumu hizo hivi karibuni ili mamilioni ya mashabiki wake katika mtandao wetu wa Spotify waweze kuburudika nazo” Alisema msemaji huyo wa Spotify japokuwa sizani kama Jay Z na Tidal watabadilisha mawazo yao.

Kwa upande mwingine Jay Z amewashangaza wengi kwa nini amechelewa kutoa albumu zake katika Apple Music, Spotify, Google Play Music na mitandao mingine mingi. Kumbuka Jay Z hapo awali alitoa albumu yake ya mwaka 1996, Reasonable Doubt (ambayo inasemekana kuwa ndio albamu yake bora zaidi) katika mtandao wa Spotify.  Albamu hiyo pia haipatikani katika mitandao mingine ukiachana na Tidal japokuwa kuna baadhi ya video zinaonekana katika mitandao hiyo.

SOMA PIA  50 Cent Aamua Kuikacha Instagram

Sema hata hivyo nina imani wapinzani wa Tidal walikua wanajua kabisa hili linakuja kwa hiyo nina imani hawajalipokea hili kwa mshangao.

Kwangu mimi kama nilivyosema ni kitu kizuri walichofanya Tidal, Niambie wewe unalipokeaje hili hapo chini sehemu ya comment. Tembelea TeknoKona kila siku. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania