Twitter imekua ikiongeza vipengele mabalimbali katika mtandao huo wa kijamii, kipengele kipya zaidi ni jinsi mtumiaji anavyoweza weka mwaka tarehe na mwezi wa kuzaliwa katika profile lake. Hii ni kitu kizuri maana watu wataweza sheherekea siku zao za kuzaliwa na wafuasi wao.
Si jambo baya watu kujua siku yako ya kuzaliwa. Pengine wakijua ndio watatafuta namna ya kusheherekea na wewe vizuri. Twitter baada ya kuongeza watuamiaji wa mtandao huo sasa wanataka ongeza vitu mbali mbali ambavyo vitawabakisha watumiaji hao ndani ya mtandao huo.
Twitter inawezesha watumiaji wake kusheherekea siku zao za kuzaliwa na marafiki na wafuasi (followers) wao. Japokuwa Twitter wameongeza kipengele hiki lakini sio lazima watumiaji wote wakitumie, kwa wale wasiotaka kutumia kipengele hiki wanaweza kuacha tuu
Sasa kwa wale wanaotaka kuweka siku zao za kuzaliwa katika ma ‘profile’ yao waende katika ukurasa wao kasha “Edit profile” “Edit profile”. Pia kwa wale ambao wanataka weka tarehe na siku ya kuzaliwa lakini sio mwaka bado twitter inawapa nafasi ya kufanya hivyo. Uonekanaji wa siku na mwezi umetenganishwa na ule wa mwaka. Mtu anaweza ficha mwaka wake wa kuzaliwa kabisa na akawa anauona yeye mwenyewe.
Kama ukienda sehemu ya “Edit profile” katika ukurasa wako utaona “Birthday” kama chaguo katika menyu itakayotokea ukibofya hapo utaona uwanja wa kujaza taarifa zako za siku ya kuzaliwa zitatokea. Pia una uwezo wa kuchagua nani aone hiyo siku yako ya kuzaliwa mfano; wafuasi wako, watu unaowafuata, wafuasi wako ambao pia unawafuata au hata uweze kuona wewe mwenyewe tuu.
Haitajalisha ni kitu gani utachofanya yaaani hata ukiweka “Only me” (mimi tuu) katika watu wa kuona siku yako ya kuzaliwa, bado Twitter itachukua taarifa zako za miaka katika kufanya matangazo yake. Usishangae maana kila tangazo lina sababu ya kufikia rika fulani hivi.
Kama ukichagua kuweka siku yako ya kuzaliwa katika ukurasa wako wa twitter, basi siku hiyo itakua ikonyeshwa kwa watu ulio wachagua tuu. Hii pia itairahisishia Twitter katika kuonyesha vitu ambavyo vinakuhusu zaidi –yaani kulingana na miaka yako kwa mfano katika matangazo—
No Comment! Be the first one.