Facebook imeamua kumruhusu kila mtu amue ni habari za aina ipi anataka kuziona kwenye kurasa yake. Hii inawezekana kwa kipengengele kipya walichokiongeza, kinachokuruhusu kuchagua marafiki wako unaopenda kuona habari zao awali ya habari zote zingine kwenye kurasa yako punde unapoingia kwenye mtandao huo wa kijamii.
Maana kuu ya badiliko hili jipya kutoka Facebook ni kwamba huna haja ya kushuka chini sana kwenye skrini ama kurasa yako kuona habari unazopenda zaidi. Hili ni jambo la kitofauti sana kutoka kwa Facebook, kampuni iliyozoeleka kuwa na usiri wa hali ya juu kuhusu namna wanavyochagua kukupa habari za marafiki na kampuni upendazo na wanafanya hivi kupitia kitu kinachojulikana kama ‘The Facebook Algorithm’ . Ili kutumia mabadiliko ya Facebook yaliyoelezwa hapa, ingia kwenye News ‘Feed Preferences’, chaguzo iliyo ndani ya menu karibu na eneo la taarifa pale juu, kulia kwenye kurasa au app yako ya facebook. Utaona orodha ya watu ma kurasa ulizoziona karibuni na zile unazozibofya kwa wingi ambazo unaweza kubadili tabia zake.
Mbali na njia hii ya kupangilia unachotaka kwa watu wengi kwa mkupuo mmoja, unaweza pia kubadili mipangilio kwa mtu au kurasa moja-moja kwa kuingia kwenye chaguzo za kila mtu au kurasa na kubadili papo kwa hapo kwenye ukurasa wako.
Ukifanikiwa kuchagua mipangilio ya kukufaa, utaweza kuona habari za hao marafiki na kurasa uzipendazo kwanza kabla ya habari za watu wengine. Kwa kweli, kwa hili la kitofauti la kutoka kwa facebook, unaweza kuona kidogo faida au labda tuseme raha, ya Facebook kwani utapata muda wote kile unachotaka.
Kwa ujumla hii ni habari nzuri, na pengine cha kufurahisha zaidi ni kwamba chaguo lako la watu unaotaka kuona ni siri yako, halitojulikana kwa wengine. Hakuta kuwa na wasiwasi kwamba mtu mwingine atajua kwamba hauwekei maanani ‘update’ zinazotoka kwake.
Je, habari hii inakugusaje wewe mtumiaji wa Facebook. Tuungane kwenye mazungumzo.
No Comment! Be the first one.