fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Maujanja

Jinsi Ya Ku’Lock’ Kivinjari Cha Mozila Kwa Kutumia Neno Siri (password)!

Jinsi Ya Ku’Lock’ Kivinjari Cha Mozila Kwa Kutumia Neno Siri (password)!

Spread the love

Kompyuta zetu tunazitumia kwa mambo tofauti tofauti hii ikiwa inajumuisha hata yale ambayo hatutaki yaonekane kwa watumiaji wengine wa kompyuta hiyo. Ndio! inawezekana ukawa unatumia kompyuta moja na mtu au hata unaweza ukaibiwa na hapo ndio taarifa zako za siri ndani ya kivinjari cha mozila zinapokuwa matatani.

Kwa mfano unaweza ukaibiwa kompyuta yako na ulikua ni mtumiaji mzuri wa mozilla kama ulikua na tabia ya kuacha mitandao yako ya kijamii bila ku ‘Sign Out’ kila unapotoka, basi kuna hati hati taarifa zako zinaweza kutumiwwa vibaya na mtu mwingine atakayetumia kompyuta hiyo.

Sasa kwanini yote hayo yatokee wakati kuna njia unaweza fanya na ikakuhakikishia usalama wa taarifa zako katika kivinjari cha mozilla?. Ili kuwezesha hili inabidi u ‘install’ Master Password+ katika eneo la Add-On. Master Password+ ni njia katika mozila ambayo itahakikisha usalama katika kivinjari chako cha mozilla

Umuhimu Wa Master Password+

– Kila utakapoingia katika kivinjari itakulazimu uweke neno siri

– Ukiachana na Kuloki Kivinjari chote, pia unaweza kuloki ‘Tabs’  mabali mbali

– Unaweza loki mara tuu ukijisikia au unaweza weka muda maalam wa kivinjari hicho kujiloki chenyewe na mengine mengi

Hatua Za Kuloki Mozilla Na Neno Siri (Password) Kwanza kabisa hii itafanya kazi katika mozila ile ya toleo la Firefox 3.6 – 39. Cha umuhimu ni kushusha toleo jipya la mozilla kama unatumia la chini ya hapo.

SOMA PIA  Mambo ya Kufanya Pale Simu au Tableti Yako Ikilowa au Kuingia Kwenye Maji

Kuiwezesha mozilla kuwa na uwezo wa kuweka loki fuata njia hizi

  • Fungua Mozilla, kisha bofya Tools -> Add-ons
  • Kibox cha Add-on Kitatokea kukiwa na sehemu ya kutafuta (search) Andika neno “Master Password” kisha bofya enter
  • Kuna matokea mengi yatatokea lakini katika hayo bofya Master Password+  kisha ibofye
  • Baada ya upakuaji na uwezeshaji kukamilika itakuaomba ku ‘restart’ kivinjari
  • Baada kufanya hivyo, fungua kivinjari chako na utaona kialama cha kufuli upande wa kulia katika kibox unachoandikia tovuti bofya hapo ili kuweka neno siri unalopendelea katika kivinjari chako cha Mozilla

make-firefox-browser-password-protected

Jinsi Ya Kukifanya Kivinjari Kiombe Neno siri  Wakati Kinafunguliwa.

  • Nenda Tools->Add-ons->Extensions katika upande wa kulia angalia Master Password+ na kisha bofya Options
  • Matokeo Yatakuja, baada ya hapo click neno ‘startup’ weka alama ya tiki kwenye “Ask for password on startup”
SOMA PIA  Uwezo wa kuwasiliana na WhatsApp moja kwa moja

how-to-lock-firefox-browser-with-password

  • Baada ya hapo kila mara utakapofungua Mozilla Firefox lazima ikuombe kuingiza neno siri

how-to-lock-mozilla-firefox-with-a-password-minKama una vitu vyako muhimu katika kivinjari cha Mozilla na hutaki viwe hadharani kwa mtumiaji mwingine wa hiyo kompyuta basi njia ni hiyo hapo juu. Ijaribu, tuambie kama imekufaa. Usiache tembelea mtandao wako pendwa kwa masuala ya teknolojia mara kwa mara. Kaa mkao wa kula juu ya Jinsi Ya Ku’Lock’ Kivinjari Cha Chrome Kwa Kutumia Neno Siri (password)!.TeknoKona tupo nawe!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania