Yandex.com – tovuti mbadala ya utafutaji kwa Google.com

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Je ushawahi kuisikia tovuti ya Yandex.com? Hii ni tovuti ya utafutaji mtandaoni kama vile Google, teknolojia yake ya utafutaji  inafanya kazi tofauti ukilinganisha na Google.

yandex.com

Yandex: Unaweza kutafuta mafaili ya aina zote

Tovuti ya Yandex ina teknolojia ya kusimamia matokeo ya unachotafuta kwa misingi tofauti ukilinganisha na ya Google. Makao makuu ya tovuti hii ni Urusi na kwa nchini humo inashika namba moja katika suala la utafutaji.

INAYOHUSIANA  Android N, toleo lijalo la Android - Fungua na tazama apps mbalimbali kwa wakati mmoja

Tovuti ya Google inapendelea matokeo kutoka tovuti zilizotengenezwa na teknolojia ya kutokoea vizuri kwenye simu, pia wanapendelea tovuti ambazo zimehakikiwa kuhusu mafaili yanayowekwa kwenye tovuti hizo. Mfano tovuti zinazowezesha watu kudownload muvi au muziki zinashushwa thamani kwenye Google katika kuonekana katika matokeo ya utafutaji (search).

Hivi ni vitu ambavyo tovuti hii haivilazimishi sana,

  • Teknolojia ya tovuti hii inaangalia zaidi usahihi wa kile unachotafuta katika kukuletea matokeo.
  • Haijalishi umri wa tovuti husika au mara ya mwisho ya tovuti hiyo kuweka vitu vipya.
  • Haijalishi kama tovuti husika ina tovuti spesheli kwa ajili ya simu au la.
  • Haijalishi umri wa makala au faili husika, Google upendelea vitu vipya zaidi
INAYOHUSIANA  App ya Wiki: ES Explorer kwa Kushughulikia Mambo Mengi kwenye Android

Kutokana na kutominya sana matokeo ya tovuti ya Yandex inapendelewa sana pia na watu ambao wanatafuta mafaili ya muvi au magemu kutoka tovuti zisizo rasmi. Tofauti na Google, Yandex itakuletea matokeo hayo pia.

Je ushawahi kuitumia tovuti ya Yandex.com katika utafutaji? Una mtazamo gani? Jaribu kutafuta kitu kwenye Google na pia kwenye tovuti hii ili uweze kujionea utofauti wa matokeo na kuona ni ipi inakufaa zaidi.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.