fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps iOS whatsapp

Polepole WhatsApp inaboreshwa kuwezesha mtu kuonyesha hisia

Polepole WhatsApp inaboreshwa kuwezesha mtu kuonyesha hisia

Spread the love

Taarifa kuhusu WhatsApp kuboreshwa na kumwezesha mtumiaji kuonyesha hisia zake kwenye jumbe zimekuwa zikielezwa mara kadhaa na sasa kipengele hicho polepole kinaonekana kuletwa kwa walengwa.

Taarifa kuhusu ujio wa kipengele kipya ambacho kinamwezesha mtumiaji wa WhatsApp kuonyesha ishara ya kucheka, kulia huzuni, n.k zimekuwa zinaelezwa na kulingana na kile ambacho WaBetaInfo imeweza kukiona inaonekana mambo yametaradadi hivyo hatupo mbali kuweza kuona kitu hicho kizuri.

SOMA PIA  Onyesha hisia za kupendezwa na ujumbe kwenye WhatsApp

WaBetaInfo wameweza kuonyesha kuwa kipengele hicho ingawa bado kipo kwenye hatua ya kujaribiwa na hjuko nyuma kuna baadhi ya watumiaji wa WgatsApp kwenye iOS wameweza kujaribu kukitumia kipengele hicho kipya.

Kwa lugha rahisi tunaposema “Uwezo wa kuonyesha hisia kwenye jumbe” ni ile hali ya mtu anakutumia ujumbe kwenye WhatsApp halafu kwa pembeni tuu chini yake upande wa kulia vinaonekana vitu vilivyo kwenye umbo la duara vikionyesha hali ya huzuni, kucheka, kuchukia, n.k.

kuonyesha hisia

Katika kile kilichoonekana ni mtu kuwa na uwezo wa kuchagua hali yanayotaka kuonyesha kwenye ujumbe alioupokea kwenye WhatsApp. Kwa idadi vipo saba.

Kipengele hicho ni sawa na tuu na vile amabavyo mtu anaweza kufanya kwenye Instagram (upande wa jumbe), Facebook Messenger ambapo mtu anaweza akachagua mchoro wa kitu fulani unaoashiria kupendezwa na kitu, huzunbi, kuchukizwa kulingana na ujumbe alioupokes kutoka kwa aliyeutuma.

SOMA PIA  NFC ni nini? Kila kitu unahitaji kufahamu kuhusu teknolojia hii

Bado haijajulikana ni lini watumiaji wote wa WhatsApp wataweza kutumia kipengele hicho na kwa taarifa zilizopo ni kwamba bado kinatengenewa. Tukusihi tuu uendelee kutufuatilia kwani tutaendelea kukufahamisha yanayojiri kwenye ulimwengu wa teknolojia.

Chanzo: WaBetaInfo

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania