Kampuni ya Apple ambao ni watengenezaji wa simu za iPhone na iPad wamewapa dili kubwa mahasimu wao wakubwa katika biashara Google, Apple wamehamishia baadhi ya huduma zao za iCloud katika mitambo ya Google.
Google ambao katika biashara ya Cloud storage hawakuwa na ushawishi mkubwa ukilinganisha na Microsoft na Amazon wanategemewa kuitumia nafasi hii kujikuza na kuongeza ushawishi wao katika sekta hii, wakati Apple nao wameamua kuwapa kazi hiyo Google lakini hawajabweteka kwani wameshatangaza kujenga Data Centres zao tatu mpya ndani ya miaka miwili.
Ingawa lina onekana kama ni jambo la ajabu kwa Apple kuwapa kazi hiyo Google ambao ni kama wapinzani wao lakini jambo usilolijua ni kwamba makampuni haya pamoja na ushindani katika baadhi ya vitengo vitengo vingine vinashirikiana saana.
Dili hili linatazamiwa kuwa litawainua zaidi Google ambao kwa sasa wanamiliki asilimia 5 tu ya soko hili, hili ni dili kubwa la pili mwaka huu kwa Google baada ya pia kupata Spotify ambao walitoka katika Amazon na kuhamia Google.
Google ambao hivi karibuni wamefanya mabadiliko mengi ili kuweza kufanya vizuri katika sekta hiyo, baadhi ya mabadiliko hayo ni kushusha bei za huduma na pia kuajiri bosi mpya mwenye ujuzi.
Chanzo: CNBC na mitandao mingine