Antonov An-225 ndio ndege kubwa zaidi duniani kuwahi kutengenezwa na inaendelea kushika rekodi ya ndege kubwa zaidi inayofanya kazi hadi sasa. Je ulikuwa unaifahamu kabla? Leo pata kuifahamu zaidi
Ndege hii ilitengenezwa na inamilikiwa na kampuni ya Antonov ambayo wakati wa ujenzi wa ndege hiyo ilikuwa ndani ya serikali ya Umoja wa Kisovyeti ila baada ya utengano ikabakia ndani ya taifa la Ukraine kwa sasa. Shirika la Antonov kwa sasa lipo chini ya serikali ya Ukraine.
Ndege ya Antonov An-225 inaurefu wa takribani mita 84 na inaweza kubeba mzigo mikubwa na kuweza kupaa ikiwa na uzito wa juu kabisa wa Kilo 640,000 yaani tani 640! Upo hapo?
Ndege hii pia inashikilia rekodi ya ndege iliyobeba mizigo mingi zaidi katika safari zake zote. Pia hadi sasa (2016) ndege hiyo inashikilia rekodi ya safari yenye mizigo mizito zaidi kwa safari moja ya ndege pale ilipobeba jumla ya mizigo ya uzito wa Kilogramu 253,820. Pia inachukulia rekodi ya ubebaji wa mzigo MMOJA mzito zaidi kwenye safari moja pale iliposafirisha mzigo wa kilogramu 189,980.
Nafasi yake ya ndani ya ndege hiyo inaweza kubeba mizigo ya hadi kilogramu 250,000 kwa safari moja.
Ilikuwaje kuwaje hadi ndege hii kutengenezwa?
Ubunifu wa ndege hii ulianza kwenye miaka ya 1980, lengo likiwa ni kwa ajili ya kusafirisha ndege spesheli ya kutumika kwa ajili ya safari za nje ya dunia (spacecraft) iliyokuwa ikifahamika kwa jina la Buran iliyokuwa inamilikiwa na Umoja wa Kisovyeti (kwa sasa Urusi (Russia)).
Antonov An-225 ilipaa kwa mara ya kwanza tarehe 21/12/1988…
Angalia picha mbalimbali zinazoonesha ndege hiyo…
Tazama video inayoonesha iruka kutoka kiwanja cha ndege
Hayo ndio mambo ya teknolojia. Ingawa ndege hii imetengenezwa miaka mingi iliyopita bado hakuna ndege iliyoifikia kwa ukubwa na uwezo wa kubeba mizigo mikubwa.
HABARI MPYA: China imeweka oda ya utengenezwaji wa ndege nyingine kama hii, kuna uwezekano mkubwa ikawa kwa ajili ya matumizi ya kijeshi. China wanategemea ndege hiyo itakayotengenezwa na kampuni ya Ukraine kuwafikia ndani ya mwaka 2019