fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Facebook Intaneti Maujanja Mtandao wa Kijamii

Jinsi ya kutumia Facebook kukuza Biashara yako

Jinsi ya kutumia Facebook kukuza Biashara yako

Spread the love

Facebook ni mtandao wa kijamii unaowezesha watu kukutana na ndugu, jamaa na marafiki mtandaoni na kutumiana picha, miziki, video, makala, pamoja na stika mbalimbali. Kuna mambo mbalimbali ambayo utatakiwa kuyazingatia kama utataka kutumia Facebook kukuza biashara yako.

Mtandao huu wa kijamii wa Facebook wenye miaka 17 sasa tangu uanzishwe umekuwa ukitumika sana na baadhi ya watu kwa ajili ya kutangaza na kuuza bidhaa zao mtandaoni na watu hao wamekuwa wakifanikiwa kwasababu soko kubwa la bidhaa siku hizi lipo mtandaoni. 

Ili uweze kutangaza na kuuza bidhaa zako ndani ya mtandao wa kijamii wa facebook ni lazima utengeneze kurasa maalum kwaajili ya biashara yako ambapo utajaza taarifa husika za bishara hiyo kama jina la duka, mahali lilipo, nembo, barua pepe yako, anuani na tovuti (kama unayo). Baada ya kufanya hayo sasa utatakiwa kuwa unatuma picha mbalimbali za bidhaa zako angalau mara 3 kwa siku katika kurasa yako ili wateja wako wasikusahau na pia ili wateja wapya waweze kuiona biashara yako.

Jinsi ya kutumia Facebook kukuza Biashara yako

Facebook hawaruhusu mtu kutengeneza kurasa ya biashara bila kuwa tayari na akaunti binafsi maana kila kurasa ya biashara lazima iwe na msimamizi mkuu ambaye huwa ndo muanzilishi wa kurasa hiyo na lazima awe ni mtu mwenye akaunti tayari facebook. Ifahamike kuwa endapo utatengeneza akaunti ya kuzugia ya facebook ili utengeneze kurasa yako kwaajili ya biashara facebook wakikugundua watakufungia akaunti hiyo pamoja na kurasa yako ya biashara na kupelekea wewe kupoteza baadhi ya taarifa zako ulizokuwa nazo awali ikiwemo na wateja wako wa mtandaoni.

Ukiwa na kurasa ya biashara yako facebook utakuwa na uwezo wa kufanya mambo mbalimbali kukuza biashara yako kama;

  • Kupata ufahamu kuhusu watembeleaji wa kurasa yako; Kwasababu utakuwa unatuma picha au video mbalimbali kuhusu bidhaa zako katika kurasa hiyo labda na kuandika makala mbalimbali kuhusu huduma unazotoa pamoja na bidhaa unazouza utakuwa na uwezo wa kuona kwanza ni watu wangapi wameona machapisho yako, wangapi walivutiwa nayo, walipenda nini zaidi kati ya vitu vyote ulivyowahi kutuma, huwa wanatembelea kurasa yako muda gani sana, watazamaji wako ni watu wa jinsia gani na umri gani na taarifa zingine nyingi.
  • Kutuma matangazo yanayowalenga wateja wako moja kwa moja; Kwanza kabisa sio lazima kuwa na kurasa ya biashara yako ili uweze kutumia huduma ya matangazo ya kulipia ya facebook hata ukiwa na akaunti binafsi unaweza kuitumia huduma hii lakini sasa kama lengo lako ni kukuza biashara yako basi huna budi kutengeneza kwanza kurasa kwa ajili ya biashara yako ndipo uanze kutuma matangazo mbalimbali kuhusu bidhaa yako ambayo yatakuwa yanawaleta watu katika kurasa yako hii ya facebook na huku wataweza kuona na kusoma kila kitu wanchohitaji kukijua kuhusu huduma zako na bidhaa zako.

Lakini pia matangazo hayo ya facebook ya kulipia yanakuwezesha wewe kama mfanya biashara kulenga aina ya watu au eneo la matangazo yako kuonekana, kwahiyo kama wewe ni muuza vipodozi basi unaweza uka chagua kuwa matangazo yako wewe yaonekane kwa wadada tu waliopo facebook.

  • Kujilinganisha na washindani wako; Facebook wameweka uwezo wa mtu kulinganisha taarifa za kurasa yake na ya mwenzake ambaye wanafanya wote biashara sawa ili uweze kujitadhmini mwenyewe kuwa ni wapi unakosea na huduma gani ambayo wewe hutoi lakini mwenzako anatoa na inamuongezea wateja? Pia utaweza kuona ni aina gani ya matangazo ambayo kwake yanapata muamsho mkubwa kutoka kwa wateja wake au kutoka kwa wafuasi wake. 
  • Kuchagua watu watakaoona machapisho yako; Hii bado ni mpya na inabidi uiruhusu kwanza kwenye kurasa yako kabla haujaanza kuitumia. Inafanya kazi kwa wewe kuchagua nani aone chapisho lako anapoingia Facebook hii unaweza kufanya kama tayari umeshalitambua vizuri soko lako na aina ya wateja ulionao katika biashara unayofanya.

Unaweza pia kujifunza mambo mbalimbali ya kukuza biashara yako mtandaoni hapa kwenye tovuti yetu kwa kutembelea kurasa hii. 

SOMA PIA  Facebook Messenger Sasa Watumiaji Bilioni 1 Kwa Mwezi! (Toleo La 2)

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania