Kwa mwaka 2015 tuu zaidi ya kondom bilioni 27 zimeuzika ila wanaharakati wanaona bado, inatakiwa ziuzike na zitumike kwa wingi zaidi ya sasa. Bado wapo wengi wanafanya mapenzi bila kutumia kondom. Ili kuweza kufanya watu wengi zaidi wafanye maamuzi ya kutumia kondom inaonekana suala la kuwa na kondom zisizopunguza raha ya tendo pale inapolinganishwa na ‘raha’ inayopatikana pale kondom isipotumika ni muhimu.
Teknolojia ya utengenezaji kondom katika suala la malighafi yanayotumika haijabadilika kwa miaka mingi sana.
Watafiti wa chuo cha Swinburne cha nchini Australia wameweza kutengeneza kondom kwa kutumia teknolojia ya kitofauti zaidi. Teknolojia hiyo inaitwa Hydrogel. Kondom nyingi zilizopo sokoni kwa sasa zinatumia teknolojia ya latex.
Hydrogels – ni mfumo wa kutengeneza malighafi ya kutengenezea kondom hizo kwa kutumia maji ambapo chembechembe za maji zinashikiliwa na ‘molecular chains’ zinazoitwa polymers.
Hydrogels zimepata sifa ya kutengeneza malighafi zenye sifa ya kukaribiana na jinsi ngozi ilivyo kwa kiasi kikubwa zaidi ukilinganisha na malighafi ya latex. Hii imesaidia kuzifanya kondom zilizotengenezwa na watafiti hao kuonekana kuweza kumpa mtumiaji karibia hali sawa na pale ambapo angefanya ngono bila kutumia kondom.
“Hydrogels zinasemekana kuwa ni malighafi inayofanana kwa ukaribu zaidi na ’tissue’ za binadamu kuliko malighafi nyingine yeyote inayotumika kwenye kondom za sasa hivi”
Je wamepata uhakika gani kuhusu ‘kiwango cha utamu’ katika malighafi ya Hydrogels?
Kwa kutumia mashine spesheli (EEG scanners), inayosoma kiwango cha furaha kwenye ubongo pale ambapo mtu ambaye macho yake yamefumbwa akashika na kupapasa vitu vya aina tofauti (malighafi). Walifanya utafiti wa kuweza kushikisha watu malighafi za aina mbalimbali na katika hizo waliweka pia malighafi ya Hydrogels – na data zikaonesha kiwango cha furaha (yaani kuona kitu kizuri sana) kilirekodiwa zaidi pale ambapo watu walikuwa wakipapasa, kushika, malighafi za Hydrogels.
Pia teknolojia hiyo imefanya iwe rahisi kwa kondom hizo kuja na dawa spesheli za kuua vijidudu kama vile vya magonjwa ya ngono kwa urahisi. Kondom ya Hydrogel itakuwa vigumu zaidi kuchanika ukilinganisha na za Latex lakini huo huo zikiwa nyembamba zaidi ya kondom za latex.
Inasemekana tayari makampuni kadhaa ya utengenezaji na uuzaji wa kondom tayari yamevutiwa na teknolojia hiyo. Suala la upatikanaji wa kondom zilizotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Hydrogels ni kati ya mwishoni mwa mwaka 2016 hadi kufikia 2017.
No Comment! Be the first one.