Kadri siku zinavyokwenda teknolojia katika simu janja (smartphones) imezidi kuboreshwa kwa viwango tofauti ili kwenda sawa na matakwa ya mtumiaji. Uboreshwaji huu pia umelenga kuhakikisha mtumiaji wa simu hizo anabaki kuwa mwenye afya bora siku zote.
Google Fit ni moja ya app zilizobuniwa kuweza kufuatilia mwenendo wa afya ya mtumiaji wa simu janja zinazotumia programu endeshaji ya Android.
App hii iliyozinduliwa mwaka jana hivi karibuni imeboreshwa zaidi na kuongezewa vipengele kadhaa ikiwamo uwezo wa kuweza kufuatilia umbali uliotembea/kimbia na kiasi cha kalori zilizotumiwa na mwili.
Ili kuongeza ufanisi wa programu hii mtumiaji atahitajika kuweka taarifa sahihi zinazomhusu ikiwemo jinsia, urefu na uzito. App hii ambayo ni nzuri zaidi kwa wale wanaojali afya zao kwa kufanya mazoezi pia ina uwezo wa kurekodi aina ya mazoezi anayofanya mtumiaji na kiwango alichofikia. Pia inakuwezesha kujiwekea malengo ya kiwango cha mazoezi unachotaka kufikia.
Kwa wale wenye saa janja (smartwatch) pia wanaweza kufaidika na app hii maana ina uwezo wa kuwasiliana na saa janja na kukuonyesha kiasi gani cha kalori ulizotumia na kiwango cha mazoezi ulichofikia.
No Comment! Be the first one.