fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti Mtandao Teknolojia

.Com Imetimiza Miaka 30: Fahamu Historia Fupi

.Com Imetimiza Miaka 30: Fahamu Historia Fupi

Spread the love

Miaka 30 iliyopita siku ya jumapili tarehe 15 machi 1985 anuani ya kwanza ya .Com ndio iliandikishwa, tukio hili lilibadilisha teknolojia ya intaneti kwa ujumla.

dot comAnuani ya ‘domain’ ya .Com haikukua kwa haraka miaka hiyo na ukiangalia hata mfumo wa ‘www.’ ulikua bado haujagunduliwa (hakuwepo kipindi hicho). Mpaka mwaka 1987 kulikua na anuani 100 tuu za .Com. Lakini kwa hivi sasa kila sekunde kuna anuani mpya ya .Com inayoanzishwa. Kwa mahesabu ya haraka kwa siku zinatengenezwa anuani za mitandao  80,000!

Mwaka 1987 ndipo makampuni makubwa yalipoanza kufungua macho na kujua kwamba teknolojia ya intaneti inaweza kutoa mchango mkubwa katika biashara zao na mchango huo utawasaidia kupata faida kwa kiasi kikubwa. Makampuni kama Apple na Sisco  kwa kufuatana walijiunga kwa kutumia ‘domain’ ya Apple.com na Sisco.com mwaka 1987.

Muonekano wa Mtandao wa Apple Miaka Hiyo Umeanzishwa

Muonekano wa Mtandao wa Apple Miaka Hiyo Umeanzishwa

Mnamo mwaka 1991  The World Wide Web (www) ilizinduliwa na kuanza kutumika rasmi. Teknolojia ya Www iliwezesha na inawezesha watu hadi leo kuweza kutumia mitandao ya dot com na mingine mingi tu kwa sasa.

SOMA PIA  Masasisho kwenye simu janja za Samsung Galaxy S20

Mwaka 1994 mtandao nguli wa Amazon ulitumia ‘Domain’  ya .Com na kuanza kutumika rasmi hiyo ni mwaka mmoja  baada ya mitandao kama Yahoo na AOL ikajiunga.  Yahoo mara ya kwanza ilianzishwa na kupewa jina la “Jerry and Dave’s Guide to the World Wide Web”na baadae ikabadilishwa na kuwa Yahoo mwaka huo huo.

Mara tuu baada ya mwaka 1996 Hotmail.com ilianzishwa na pia hata Expedia.com ambayo ilibadilisha kwa kiasi kikubwa jinsi ya kukata tiketi za safari ki mtandao.

SOMA PIA  HongMeng OS: Kufanya kazi kwenye kompyuta, simu, tableti na vifaa vingine

Mwaka 1997 Netflix.com ilianzishwa na baada ya mwaka Google.com ikawa hewani na kubadilisha jinsi ya kupata taarifa mbali mbali katika mtandao (Intaneti).

Mitandao mingine mikubwa iligunduliwa  mfano Skype.com ilianzishwa mwaka 2003 ambayo inahusisha kupiga na kupokea simu kimtandao (online). Mwaka 2004 Thefacebook.com ilianzishwa ambayo baadae ilibadilishwa jina na kuwa facebook.com. Youtube,Com ilienda hewani mwaka 2005 na baada ya mwaka tuu mtandao wa Twitter.com ukawa hewani tuu.

Heri ya kuzaliwa .com  🙂

Tafadhali ungana nasi pia kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania