fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Tablet Teknolojia

SecuTABLET : BlackBerry, Samsung na IBM Waungana Kuleta Tableti

SecuTABLET : BlackBerry, Samsung na IBM Waungana Kuleta Tableti

Spread the love

Miaka kama mitatu minne hivi iliyopita mtu asingefikiria kuna muungano kama huu ungeweza kutokea katika kuleta kifaa chochote kama tableti. Lakini umetokea.

Baada ya BlackBerry kununua kampuni moja ya teknolojia ya kiusalama zaidi ya Secusmart ya huko Ujerumani sasa wameshirikiana na kampuni ya IBM na Samsung na kuleta tableti iliyo kwenye kiwango cha juu kabisa cha kiusalama inayoenda kwa jina la SecuTABLET.

secusmart-blackberry-samsung-ibm

SecuTABLET imetumia tableti ya Samsung Galaxy Tab S 10.5 kujengea mfumo wake wa juu wa Kiulinzi/Usalama

Tableti hiyo ambayo itaweza kutumiwa na vitengo muhimu vya kiserikali na makampuni au mashirika kama ya kibenki n.k ambayo ni muhimu masuala/data zake zitunzwe kwa usiri mara zote kuzilinda kutoka kwenye wizi wa kiintaneti – yaani ‘hacks’.

Tableti hii itatengenezwa kutumia toleo la Samsung Galaxy Tab S 10.5 na teknolojia ya ulinzi iitwayo ‘secure app wrapping’ kutoka IBM.  Apps za kawaida kama vile Facebook, YouTube, Twitter na WhatsApp pia zinaweza kutumika bila wasiwasi wowote wa kiusalama.

Chini ya Uongozi wa Bwana John Chen, BlackBerry Imebadilika Kutoka Kutegemea Mapato ya Mauzo ya Simu na Kujikita Zaidi katika Teknolojia ya Usalama/Ulinzi

Chini ya Uongozi wa Bwana John Chen, BlackBerry Imebadilika Kutoka Kutegemea Mapato ya Mauzo ya Simu na Kujikita Zaidi katika Teknolojia ya Usalama/Ulinzi

Kampuni ya BlackBerry inajikita zaidi katika masuala ya teknolojia ya usalama na inasemekana imeanza kuona mapato yake yakikua zaidi taratibu. Kampuni ya teknolojia ya usalama ya Secusmart waliinunua mwezi wa kumi na mbili, 2014 na pia tayari kwa ushirikiano na Samsung, BlackBerry wametoa programu inayoweka ulinzi zaidi kwa simu na tableti za Samsung Galaxy inayotambulika kama ‘BlackBerry Enterprise Service 12’.

SOMA PIA  YouTube Waleta Video za 'Virtual Reality': Sasa Tazama Video kwa Nyuzi 360

Bado hawajasema rasmi tableti hii ya SecuTABLET inataingia lini sokoni ila wameshaeleza ni itakuwa inauzwa bei ya juu zaidi kutokana na teknolojia iliyotumika na aina ya wateja wanaotegemewa kuitaji kifaa kama hichi.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania