fbpx
Apple, IPhone, simu, Teknolojia

Vidokezo vya iPhone XR 2019

vidokezo-vya-iphone-xr-2019
Sambaza

Mara kadhaa tangu kuanza kwa mwaka mpya apple wameingia kwenye vichwa vya habari kuhusiana na simu janja ambazo itazindua mwaka huu kwa mara nyingine tena kuna taarifa kuhusu iPhone XR ya mwaka 2019 zitakavyokuwa.

Wakati simu za iPhone za mwaka 2018 zinatoka wachambuzi wengi/wanahabari wa masuala ya teknolojia waliita iPhone XR “Simu ya wengi” kutokana na sababu mbalimbali mara baada ya kuilinganisha na nyinginezo zilizotoka siku moja chini ya mwamvuli wa kampuni moja (Apple). Sasa je, hii ya 2019 ikoje?.

INAYOHUSIANA  Soko la apps za Android, Google Playstore kupatikana kwa watumiaji wa Chrome OS

Kwa muonekano

Kiujumla toleo la sasa ambalo bado halijatoka na lile la mwaka ulioisha mabadiliko ni asilimia 50 kwa 50 ambapo iPhone XR 2019 inaonekana kuwa nyembamba zaidi kutokana na kwamba wembamba wake ni mm 7.8 wakati ile ya mwaka jana ni mm 8.3. Kwa upande wa uso wa mbele simu hii inayoizungumzia haijabalika sana kwani itakuwa na kioo henye urefu inchi 6.1.

Eneo la kamera

Ingawa hakuna undani kamili unafahamika kuhusiana na ubora wa kamera husika lakini kutokana na kwamba Apple hawajabadilisha muonekano wa uso wa mbele (kwa kamera ya mbele) pengine wakatumia sifa zilezile zilizopo kwenye iPhone XR iliyopo madukani sasa hivi. Upande wa nyuma kunaonekana kuwepo na mabadiliko madogo kwa kamera hizo ambazo ni mbili kwa idadi kuonekana katika umbo la mraba.

INAYOHUSIANA  Fahamu Kuhusu Viatu Janja Kutoka Lenevo! #Teknolojia
iPhone XR 2019
Kamera za kwenye iPhone XR 2019 ambazo huenda zikawa na MP 12 kila moja ambapo zitapatikana katika rangi sita tofauti.

Sehemu ya kuchomeka kimemeshi

Zipo taarifa kuwa Apple watahamia kwenye teknolojia ya USB-C (USB Type-C) ambapo zitaruhu watumiaji wake kutumia kimemeshi (chaji) chenye 18W lakini bado kuna mashaka makubwa kwa teknolojia hiyo kuoonekana hasa kwenye iPhone XR 2019.

Vilevile, inaaminika kuwa iakuwa/zitakuwa ni simu janaja za mwisho kutoka Apple kutumia teknolojia ya LCD kwenye kioo na kuhamia kwingine lakini kwa sasa hakuna anayeweza kusema mengi mpaka hapo simu/bidhaa chini ya kampuni hiyo zitakapotoka baadae mwaka huu na miaka mingine ijayo.

Vyanzo: GSMArena, MacRumors

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|