fbpx
Teknolojia

Japan: Kibanika Mkate kinachouzwa kwa zaidi ya Tsh 600,000

japan-kibanika-mkate-kinachouzwa-nusu-milioni
Sambaza

Wajapani kama vile wazungu, wanapenda sana kutumia kibanika mkate kwenye kuandaa mikate yao. Tendo la kubanika mkate (yaani toast) ni la umuhimu sana kwao kiasi kwamba kampuni moja imekuja na mashine inayouzwa kwa bei ya zaidi ya nusu milioni.

Kwa miaka kadhaa sasa nchini Japani na mataifa mengine kumekuwa na umaarufu wa vifaa vipya vya kisasa vya ubanikaji mikate.

INAYOHUSIANA  Tigo kuwabadilishia simu wenye simu feki! #Ofa

Kifaa cha ‘toaster’ kina kazi moja tuu – kuchoma mkate katika ubora/kiwango flani, na kutumia zaidi ya laki 6 katika ununuaji wa kifaa kama hicho kwa wengine inawezekana ikawa ni utumiaji mbovu wa pesa. Kwa wapenda mikate inayopitia hatua hii pesa hii inaweza kuwa ni jambo la kawaida tuu, tayari kuna vifaa hivyo vingine vinavyouzwa kwa bei karibia na hiyo.

mitsubishi kibanika mkate

Kibanika Mkate kutoka Mitsubishi
Kibanika Mkate kutoka Mitsubishi: Kwa bei ya takribani laki 600,000

 

INAYOHUSIANA  Xiaomi Mi Mix 3 yenye 5G imetoka

Kibanika mkate hiki kimetengenezwa na kampuni ya Mitsubishi – Mitsubishi Electric Corp. Ingawa mara nyingi vifaa hivi vinakuwa na uwezo wa kupokea zaidi ya kipande kimoja cha mkate, machine hii imepewa uwezo wa kupokea kipande kimoja tuu.

Wenyewe Mitsubishi wamesema wamefanya hivyo ili kuhakikisha ubora wa hali ya juu katika kipande kimoja – kuliko kuwa na uwezo wa kupokea vipande vingi huku ubora ukiwa si mzuri.

INAYOHUSIANA  Maana ya "TTY Mode" kwenye rununu
mitsubishi kibanika mkate
Muonekano wa mkate baada ya kubanikwa kwenye kifaa hichi

Je una mtazamo gani kuhusu kifaa hichi? Je mkate una thamani gani kwako?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |