Marekani huenda ikazidisha katazo la utumiaji wa Laptop ndani ya ndege, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters huenda abiria wa ndege zote za kimataifa kwenda Marekani hawataruhusiwa kuingia na Laptop ama vifaa vikubwa vya elektroniki ndani ya ndege.

Msemaji wa Idara ya mambo ya ndani wa Marekani David Lapan amethibitisha hayo wakati akiongea na kamishna wa mambo ya ndani wa Ulaya, Â anasema ingawa bado mpango huo haujatangazwa lakini upo mezani.
Pia katika mahojiano na kituo cha Fox News John Kelly ambaye ndiye waziri wa ndani wa usalama wa Marekani amesema kwamba Marekani inapanga kuongeza kiwango cha usalama wa anga ikiwa ni pamoja na kuongeza ukaguzi wa vifaa vinavyo bebwa na abiria kuingia navyo ndani ya ndege.
Mwezi Machi Marekani iliweka katazo la kuingia na Laptop pamoja na vifaa vingine vya elektroniki katika ndege kwa ndege zinazotoka viwanja kumi, nchi zilizokumbwa na katazo hilo ni pamoja na Uturuki na baadhi ya nchi za kiarabu.