fbpx

Google, Google Pixels, simu, Uchambuzi

Simu ya Pixel 3A na 3A XL – Google waja na Simu ya Pixels kwa bei ‘rafiki’

google-simu-ya-pixel-3a-3axl-uchambuzi

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Google watambulisha Google Pixel 3A na 3A XL katika kongamano lao kubwa la Google IO linalohusisha watafiti na waandishi habari muhimu katika sekta ya bidhaa za teknolojia.

Siku chache zilizopita Google wametambulisha Google Pixel 3A na 3A XL katika kongamano lao kubwa la Google IO linalohusisha watafiti na waandishi habari muhimu katika sekta ya bidhaa za teknolojia.

Simu ya Pixels 3A
Simu ya Pixels 3A

Katika simu ya hizi Google wamefanya mabadiliko machache ukilinganisha na toleo lililopita la Pixel 3, kikubwa ikiwa kwenye eneo la bei na hivyo kuondolewa kwa baadhi ya sifa. Wamezileta katika bei inayoonekana ni nafuu zaidi kwa simu za kisaa za Google Pixels, simu za Pixel 3A zinaanza kupatikana kwa takribani Dola $400 ambapo inamaanisha ni takribani milioni 1 za kitanzania.

Sifa za Google Pixel 3A

Ingawa inapatikana kwa takribani nusu ya bei ya toleo lililopita la Pixel 3, bado simu ya Pixel 3A inakuja na kamera yenye uwezo mkubwa ikibeba sifa kadhaa kutoka toleo lililopita.

Moja ya sifa kubwa kwa mtu utakayenunua simu hizi ni pamoja na uhakika wa kupata masasisho (updates) ya matoleo mapya ya Android kwa wakati bila kuchelewa katika kipindi cha miaka mitatu.

 • Inakuja na disk ujazo ya GB 64
 • Inakuja na prosesa ya Snapdragon 670
 • Diski uhifadhi wa GB 64
 • Teknolojia ya eneo la kuchomeka earphone – headphone jack.
 • Toleo kubwa la Pixel 3A linakuja na display/kioo cha Full HD OLED cha ukubwa wa inchi 6 wakati ndogo ni ya ukubwa wa inchi 5.6
 • Toleo kubwa yaani, Pixel 3A XL linakuja na betri la mAh 3,700 wakati la 3A linakuja na betri la mAh 3,000.

Toleo hili la Pixel halitakuwa na uwezo wa kuzuia maji (water resitance) na uwezo wa kuchaji bila waya (wireless).

Teknolojia ya kuchaji bila umeme ambayo ilikuwepo kwenye toleo lilolopita (Pixel 3) imetolewa, teknolojia ya wireless charging huwa inapatikana kwenye simu zenye sifa ya bei iliyo juu kuliko hii. Na inaonekana Google wameona sio mbaya kuacha na teknolojia ambazo zingeongeza gharama katika utengenezaji wa simu.

SOMA PIA  Jinsi Ya Kusafisha Kioo Cha Simu Janja!
Simu ya Pixels
Simu ya Pixels 3a: Inakuwa moja ya simu ya kwanza kuja na teknolojia mpya za Android. Hii ni katika app ya Google Maps ambapo utaweza kuelekezwa unapoenda kwa kutumia teknolojia ya kamera yako, AR na 3D

Kamera;

google pixel 3a
Simu ya Google Pixel 3a

Teknolojia katika kamera ya nyuma: 

 • Megapixel 12.2 (dual-pixel)
 • Yenye uwezo mkuwa wa kugundua vitu na kukusaidia kwenye kufocus (Autofocus) pamoja na uwezo wa kupiga picha nzuri ata pale picha inapopigwa wakati wa mitikisiko (electronic image stabilization)
 • ƒ/1.8 aperture
 • Teknolojia katika urekodi wa video (1080p @ 30fps, 60fps, 120fps; 720p @ 30fps, 60fps, 240fps pamoja na
  4K @ 30fps)
SOMA PIA  Pesa Inayotengenezwa Na Apple, Facebook Na Wengine Ndani Ya Sekunde!

Teknolojia katika kamera ya selfi:

 • Megapixel 8
 • f/2.0 aperture
 • Teknolojia katika urekodi wa video (1080p @ 30fps, 720p @ 30fps, 480p @ 30fps)

Simu hii ni nzuri na ni ya kisasa na kwa eneo la kamera simu za Google Pixel ni simu zenye kiwango cha juu sana cha ubora. Kwa kuwa na simu yenye uwezo wa huu kwa bei hii inaonekana Google wanataka kuvutia watumiaji wengi zaidi katika familia ya simu za Google Pixel.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Comrade Mokiwa

Comrade MokiwaMuanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COMMuda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri@teknokona.com |