fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Air Tag AirPods Apple Teknolojia

Mfuko unaoweza kutunza Air Tag na AirPods Pro kwa pamoja

Mfuko unaoweza kutunza Air Tag na AirPods Pro kwa pamoja
Spread the love

Usalama wa vitu vyetu vya kidijitali ni muhimu sana hasa ukizingatia ulimwengu huu buliotawaliwa na teknolojia ambapo bidhaa nyingi ni ghali. Ni kitu kizuri kama inawezekana kutunza Air Tag na AirPods Pro sehemu moja.

Wengi wetu tunafahamu bei ya AirPod Pro; kwa kifupi tuu ni ghali lakini pia ni ndogo kwa umbo kiasi kwamba kuwa rahisi kupotea hivyo kuleta majonzi kwa aliyepotelewa/kuibiwa. Pengine hii inaweza kuwa ndio sababu kuu ya kuwafanya Apple kutengeneza kifaa kidogo ambacho kinaweza kufuatilia bidhaa fulani iwapo Air Tag ipo karibu na bidhaa husika ambayo mtu asingependa kuipoteza.

Air Tag

Air Tag inasaidia kumwambia mtu mahali ambapo kifaa chake kilipo iwapo vyote viwili vipo pamoja na kimeunganishwa na simu janja.

Halikadhalika, kwenye AirPods Pro kuna ubunifu mpya umefanyika ambapo mfuko huo unaweza kutunza vitu hivyo viwili kwa pamoja na usalama. Mfuko huo uitwao Tag Armor Duo unauzwa $35|zaidi ya Tsh. 80,500 bei ya ughaibuni inaweza kukupa hafueni ya kujua zilipo AirPods Pro ambapo zinauzwa $249|zaidi ya Tsh. 572,700 kutoka kwa Apple wenyewe.

Air Tag

Tag Armor Duo: mfuko ambao una nafasi ya kutunza Air Tag na AirPods Pro sehemu moja.

Hii ni bidhaa ambayo kiukweli inavutia na hata kushawishi kuinunua hasa kwa sisi ambao tunapenda kuburudika kwa muziki mzuri kupitia simu janja zetu. Karibu ewe msomaji wetu kutupa maoni yako kuhusiana na bidhaa hii.

Vyanzo: Engadget, mitandao mbalimbali

SOMA PIA  Kingo Root: Programu/App ya Kuroot Simu za Android na Windows

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania