fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Google Magari Teknolojia

Google: Magari Yetu Ya Kujiendesha Yenyewe Yamepata Ajali Mara 11 Tuu!

Google: Magari Yetu Ya Kujiendesha Yenyewe Yamepata Ajali Mara 11 Tuu!

Spread the love

Kama wewe ni mfuatiaji mzuri wa Teknolojia hasa zile za makampuni makubwa huwezi liacha kampuni kubwa, Google. Na tukizungumzia kampuni ya Google ukiachana na teknolojia zake zingine ipo hii ya kuvutia kuhusiana na gari inayojiendesha bila dereva kuwa nyuma ya usukani.

Sawa tumesikia mengi ya ajabu kama vile gari isiyotumia mafuta n.k lakini hii ni ya ajabu zaidi ila kwa teknolojia ya kisasa ni jambo linalowezekana.

3ecda5dab3d61c3c_14503213895_7712140b04_o.xxxlarge_2x

Muonekano ya moja ya magari hayo yanayojiendesha yenyewe!

Najua kuna maswali mengi unaweza kujiuliza je ni vipi gari inafanya kazi (kuweza kujiendesha yenyewe) ukiwa na swali hilo hilo kumbuka pia teknolojia inakua kwa kasi sana. Google ni moja kati ya makampuni machache duniani yaliyo juu katika maswali ya ubunifu katika nyanja ya Teknolojia.

SOMA PIA  Google Inanunua Sehemu Ya Timu Nyuma Ya Simu Za HTC!

Google ilisema katika makala kwenye blog  kuwa ajali zilizotokea kwa magari ya teknolojia hiyo ni  tuu katika kipindi cha miaka sita (6).  Ajali zote zilizotokea ni ndogo ndogo na zinazo pelekea taa kuvunjika.  katika blog mwendeshaji wa programu ya gari zinazojiendesha zenyewe wa Google, Chris Urmson alisema kuwa Ajali huwa zinatokea kwenye gari wakati gari inaendeshwa na dereva mwingine wakati inajiendesha yenyewe.

Makala ya  Urmson  ilitoka siku moja na ripoti ya Associated Press (AP) ikiwa inaripoti kuwa magari manne (4) ya kujiendesha yenyewe yameonekana katika ajali California tangia mwezi septemba. Tatu kati ya hizo ni magari ya kujiendesha yenyewe toka Google na gari lingine ni lile linalomilikiwa na Delphi, kampuni kubwa inayosambaza magari.

Magari ya kujiendesha yenyewe kutoka Google yanafanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza kabisa California na Nevada.

 Angalia Video Ifuatayo Kufahamu Zaidi Kuhusu Gari Hizi Kutoka Google

Gari hizi zinapunguza ajali barabarani kwa kiasi kikubwa na sio kwamba haziendeshwi na walevi hapana! ni kwa sababu zinawekewa teknolojia ya hali ya juu sana.  Hebu fikiria gari hii inaweza tofautisha mtembea kwa miguu na muendesha baiskeli pia hata gari ya abiria na isiyo na abiria. Pia usisahau kuna ajali 11 tuu kwa kipindi cha miaka 6, Kuna baadhi ya watu wanaweza amini zaidi gari hii kuliko madereca wao wa siku zote.

Toa mawazo yako sehemu ya Comment Pia tembelea kurasa zetu za Twitter, Facebook Na Instagram

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania