Kama njia mojawapo ya Tanesco kuwa karibu na kuweza kujua kero za wateja wake shirika hilo wameanzisha makundi kwenye WhatsApp.
Ukitaka kutoa huduma iliyo bora kwa umaa basi ni vyema sana kuwa karibu na watu wako. Ndio, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetengeza makundi kwenye WhatsApp ili kuweza kupata taarifa kuhusu matatizo ya umeme kutoka kwa wanaowahudumia.
Kwa mujimu wa agizo kutoka kwa wajumbe wa bodi ya Tanesco shirika hilo linapaswa kutengenza makundi kwenye WhatsApp ngazi ya wilaya na mikoa Tanzania nzima.
Makundi hayo ni kulingana na aina ya wateja kwa maana ya kwamba wateja wakubwa/wawekezaji wengine wakiwa wa kawaida kuanzia ngazi ya mtaa hadi mkoa.
Nini lengo la TANESCO kuanzisha makundi ya kwenye WhatsApp?
Kwenye nchi yoyote suala zima la upatikanaji wa nishati ya umeme ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa nzima. Tanesco wamekuwa lawamani kutokana na matatizo umeme, sasa makundi hao ndani ya WhatsApp yanalenga:-
- kutoa na kupokea taarifa za nishati ya umeme kwa wateja wao wa kanda mbalimbali nchini,
- kuhakikisha wateja wanapata taarifa ya kila kinachoendelea kuhusu nishati ya umeme.
Nani atakuwa kiongozi wa kikundi?
Ili mambo yaweze kusonga na kuleta matokeo chanya ni lazima awepo kiongozi hivyo basi Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la umeme Tanzania katika mtaa anaoishi ameunganishwa kama mteja wa Tanesco kwenye kundi la WhatsApp na wakati huo huo kama kiongozi.
Makundi hayo yatajumuisha wateja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Tanesco lengo ni kuhakikisha changamoto yoyote inayohusu umeme inatolewa kwa wakati.
Chanzo: Mtanzania