Simu janja nyingi zimekuwa zikipata matatizo ya kuvunjika kioo cha mguso na kuifanya simu kuwa na kasoro ambayo inaweza kusababisha simu hiyo isiweze kufanya kazi vizuri/ikafanya kazi vizuri lakini muonekano wake usiwe wa kuvutia tena kama ilivyokuwa hapo zamani.
Na vipi pale umeidondosha simu janja na kioo cha mguso kikapata dosari na kusababisha simu kutofanya kazi ipasavyo? Kuna mbinu ya kutumia ili kuweza kutumia simu yako ambayo imepata dosari kwenye kioo.
TeamViewer ni programu wezeshi/tumishi inayosaidia mtu kuweza kufikia kile kilichohifadhiwa kwenye simu/kompyuta bila ya kuwa karibu na kifaa husika; kuna mawasiliano kati ya vifaa viwili au zaidi.
TeamViewer inafanyaje kazi?
Kitu cha msingi kabisa na muhimu katika kufanikisha TeamViewer ifanye kazi ni kujua tarakimu zilizotokana na baada ya kuweka TeamVuewer kwenye kompyuta/simu na kisha utambulisho (ID) huo ukausambaza kwa kifaa kingine ili kuweza kutengeneza mawasiliano kati ya vifaa vyenu.
Si makampuni yote ya simu yanaruhusu kuweza kufanya kila kitu kwenye kile kifaa kingine lakini kwa makampuni kama Samsung, Motorola, LG, Sony, Apple yanaruhusu kuweza kuona na kuhamisha kitu/vitu kutoka kwenye kifaa husika kwenda kwenye kifaa kingine.
Utambulisho wa kifaa kingine (partner) ndio utakuwa mwanzo wa kuweza kufikia simu/kimpyuta kutokana na mawasiliano kati ya vifaa hivyo viwili yanakuwepo.
Namna ya kutumia TeamViewer.
1. Shusha na hifadhi (install) TeamViewer QuickSupport kwenye simu yako. Pia unaweza kupakua TeamViewer Hostlakini itakuhitaji kuweza kuingia (sign in) kwenye simu yako kwa kutumia barua pepe/neno siri la kwenye TeamViewer. TeamViewer Host haihitaji usambaze ID yako kwa mwingine.
2. Fungua TeamViewer QuickSupport na hapo utaweza kuona tarakimu maalum ambazo ndio utambulisho wa kifaa chako. Unaweza kuzinakili au ukazituma kwenda kwenye barua pepe yako kwa sababu ni muhimu sana kuwa nazo.
TeamViewer: Utambulisho wa kifaa husika (ID) ambao unatumika kutengeneneza mawasiliano kati ya vifaa viwili au zaidi.
3. Kupitia kompyuta, tembelea start.teamviewer.comkisha weka namba ya utambulisho wa kifaa ambacho unataka uwe na uwezo wa kuwa na mawasiliana (kuona, kutuma/kupokea data) kisha bofya Connect to Partner. Kama utakuwa TeamViewer haipo kwenye kompyuta itaanza mara moja kuishusha.
4. Kama TeamViewer tayari upo kwenye kompyuta cha kufanya ni kufungua TeamViwer ya kwenye kompyuta kisha kuweka ule utambulisho wa kifaa ambacho unataka kukiunganisha na kompyuta kisha unabonyeza Connect.
5. Ingia kwenye simu na kisha bonyeza Allow kuruhusu mawasiliano kati ya vifaa hivyo. Hapo utaanza kuona kila kitu kilichopo kwenye uso wa mbele wa simu yako na kama simu hiyo inaruhusu kuhamisha mafaili kuweka au kuondoa apps, picha, n.k utaweza kufanya hivyo vinginevyo utakuwa na uwezo wa kuona tu.
Kwa ushauri wa bure kabisa, ni vyema ukaweka TeamViewer kwenye simu yako mapema kabisa wakati simu yako haijakumbwa na matatizo ya kuharibika kioo au matatizo mengineyo ili kuwa na uhakika wa kuikia vitu vya kwenye simu wakati wowote.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|