Smart Beauty Mirror: Kioo Janja Kwa wadada walimbwende wenye kujali muonekano wao

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Umeshawahi kumuona mtu aliyejiweka ‘make Up’ usoni tena kwa kutumia kioo na akawa kichekesho kwa wengi? Aidha kwa kujiweka poda zilizopita kiasi au kuonekana kama mwenye ngozi iliyochafuliwa badala ya kupambika? Smart Beauty Mirror ni msaada kwa wadada walimbwende.

Basi kwa wale ambao wameshawahi kukutana na kadhia hiyo, wameletewa suluhisho kwa kioo Janja (Smart Mirror) kinachofahamika kama Smart Beauty Mirror kilichobuniwa na Kampuni ya HiMirror ambao ni wataalamu masuala ya ngozi na mwili.

INAYOHUSIANA  Spika yenye sehemu ya kuwekea bilauri

Kwa wale wenye kupenda masuala ya ulimwende wa sura zao na kujikagua kabla ya kutoka basi
kioo janja hiki ni ajili yao kitakachowasaidia kazi ya kijiremba kuwa urahisi na uhakika zaidi.

  • Kioo hiki kina kamera ambayo hutathmini kila sehemu ya ngozi yako hususani kwenye uso.
  • Kitakuonesha ikiwa ngozi imejikunja, imeparara, hujapaka mafuta vizuri au ikiwa kuna kovu ambalo huenda likakuharibia muonekano wako mzuri.
  • Pia kitakushauri namna ya kuuremba uso wako kulingana na wakati gani. Kama ni Make Up kwa ajili ya muda wa Asubuhi, mchana, Jioni au usiku.
  • Kadhalika, hukufahamisha ikiwa ngozi yako ina matatizo ya kiafya na kukushauri kumwona daktari.
HiMirror Smart Beauty Mirror

Smart Beauty Mirror: Kioo hicho kinakuja na kamera na app yake ndani yake. Utaweza kupata taarifa mbalimbali kuhusu ngozi na urembo.

Kioo Janja hiki kilianza kuuzwa Jualai 2018 tayari kinapatikana kuuzwa kupitia mtandao wa Amazon kwa kiasi cha Dola za Marekani 149 ambazo ni sawa na Tshs 343,000/-

Haya sasa kwa wale madada wenye uraibu wa ulimbwende wakakinunue kwa ajili ya ufanisi wa urembo wa sura zao.

Tovuti ya mtengenezaji: HiMirror
Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.