fbpx

Facebook, Intaneti

Muonekano Mpya wa Facebook kwa watumiaji wa Kompyuta

muonekano-mpya-wa-facebook-kwa-watumiaji-wa-kompyuta

Sambaza

Kwa muda mrefu Facebook waliweza baridi muenekano wa mtandao wao kwa watumiaji wa tovuti hiyo kupitia app ya simu, na sasa watumiaji wa kompyuta wakumbukwa.

App yao imekuwa na muenekano mzuri na wakuvutia kwa wateja wao. Kwa sasa Facebook wameweza kuleta mabadiliko pia kwenye tovuti yao kwa ajili ya watumiaji wa kompyuta.

Muenekano huu umekuwa kama unaendana na wasimu kitu ambacho wengi wamefurahia kwa hujio wake.

Muonekano Mpya wa Facebook
Muonekano Mpya wa Facebook

Jinsi ya kubadili kutoka muenekano wa zamani kwenda Mpya.

  • Ukiwa katika page yako kwa upande wa kulia kuna mchale unaotizama chini , Bonyeza hapo alafu shuka mpaka chini alafu bonyeza kwenye “Switch to New Facebook
SOMA PIA  Janga la Ebola: BBC kutoa taarifa kwa WhatsApp

Muonekano Mpya wa Facebook

  • Baada ya hapo kama ni mara ya kwanza utaletewa ukurasa kama huo chini alafu utabonyeza “Next

  • Baada ya hapo utaletewa ukurasa wa kuchagua mueneokano kati wa usiku au mchana yaani “dark mode au light¬† mode

  • Baada ya hapo mwisho kabisa sasa unapewa ukurasa wa kuchagua namna gani ukurasa wako utakavopangiliwa
SOMA PIA  Korea Kaskazini wakana kuiba zaidi ya trilioni 4.6 kwa njia ya mtandao. #Udukuzi

Muonekano Mpya wa Facebook

Baada ya hapo sasa ndo utakuwa umefanikiwa kuweza kuruhusu muonekano mpya wa Facebook ndani ya akaunti yako kupitia kifaa chako cha kompyuta.

Pia muonekano umebadilika kila mahali na kukufanya uweze kubadili taarifa zakokwa urahisi, pia unaweza kutuma ujumbe kwa marafiki kwa urahisi na mbali na hayo unaweza kuangalia “status” za marafiki zako kwa urahisi kupitia muonekano huu mpya wa facebook katika kifaa cha kompyuta.

SOMA PIA  Jinsi Ya Kulinda Taarifa Na Kuifanya Akaunti Yako Ya Facebook Kuwa Ya Kibinafsi!

Baadhi ya Screenshots zinazoonyesha muonekano mpya wa Facebook.

Ukurusa wa status

muonekano mpya wa facebook

Ukurasa wa Akaunti ya mtumiaji wa Facebook

Kama unahitaji kurudi kwenye muenekano wa zamani basi unarudi pale pale kwenye mshale wa upangiliaji (setting) unaolekea chini alafu unabonyeza “Switch to Classic Facebook” utakuwa umerudi kwenye muenekano wa zamani.

muonekano mpya wa facebook

Je, unauonaje muonekano huu mpya wa Facebook kwa watumiaji wa Kompyuta?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Lymo

A Cyber Security Guy | A student | I Know A lot