fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Intaneti Mtandao wa Kijamii simu Teknolojia Twitter Uchambuzi

Twitter inaripotiwa kuwa ilijua Twitter Spaces inaweza kutumika vibaya kwa sababu ya ukosefu wa usimamizi

Twitter inaripotiwa kuwa ilijua Twitter Spaces inaweza kutumika vibaya kwa sababu ya ukosefu wa usimamizi
Spread the love

Twitter, mtandao wa kijamii wenye wastani wa watumiaji milioni 206 kwa mwezi, umeripotiwa kufahamu na kupuuzia madhara ya huduma yao mpya ya Twitter Spaces inayowezesha watumiaji kufanya mazungumzo ya sauti ya moja kwa moja.

Tangu kuanzishwa kwa Spaces mapema mwaka huu, mamia ya watu wameripotiwa kujiunga na mijadala hii ya moja kwa moja ya sauti inayoongozwa na “wafuasi wa Taliban, wazalendo wa kizungu, na wanaharakati wa kupinga chanjo wanaopanda habari potofu za coronavirus.” Kulingana na The Washington Post, Twitter haikuwa na zana za kudhibiti zinazohitajika kukabiliana na unyanyasaji, wito wa vurugu na matamshi ya chuki katika Spaces.

SOMA PIA  Simu milioni 900 za Android hatarini kudukuliwa

Spaces haina wasimamizi wa kibinadamu au teknolojia inayoweza kufuatilia sauti katika wakati halisi. Ni vigumu zaidi kukagua sauti kiotomatiki kuliko maandishi. Kufikia sasa, Twitter imeegemea jamii kuripoti Spaces wanazofikiri zinakiuka sheria za kampuni. Kulingana na ripoti hiyo, teknolojia ya Twitter ilisaidia baadhi ya mijadala hii kusambaa. Kwa sababu Spaces hizi zilikuwa zikikusanya hadhira kubwa, mifumo ilizielewa kuwa maarufu, na kuzikuza kwa watumiaji zaidi.

Twitter Spaces

Picha: Muonekano wa Twitter Spaces

“Kuhakikisha usalama wa watu na kuhimiza mazungumzo yenye afya, wakati huo huo kusaidia waandaji na wasikilizaji kudhibiti uzoefu wao, kumekuwa vipaumbele muhimu tangu mwanzo wa maendeleo ya Spaces,” Msemaji wa Twitter Viviana Wiewall alisema.

SOMA PIA  Uchambuzi wa Tecno Spark 5, Uwezo na Sifa.

Chanzo: Engadget na vyanzo vingine.

Teknokona tunaendelea kufuatilia kwa kina kuhusu njia itakayopatikana ya Twitter kusimamia mijadala ya sauti inayofanyika kupitia huduma yake ya Twitter Spaces na kukujulisha. Endelea kutembelea tovuti yetu kufahamu zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake na pia kupata habari mbalimbali za kiteknolojia. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania