fbpx
Apple, IPhone, simu, Teknolojia

iPhone 12 Pro Max na picha zake za awali

iphone-12-pro-max-na-picha-zake-za-awali
Sambaza

iPhone 12 Pro Max ni moja ya simu zinazotengezwa na Apple ambazo zinategemewa kuzinduliwa baadae mwaka huu na kama ilivyo kawaida upo mtindo wa kupata tetesi mbalimbali kuhusu rununu/bidhaa kabla ya kutoka rasmi.

Ni desturi ya kampuni tajiri namabari moja kwenye masuala ya teknolojia kufanya uzinduzi wa bidhaa zake mbalimbali mwezi Septemba lakini kabla ya kufika huko tayari tovuti mbalimbali zimeshaweza kupata taarifa kadha wa kadha kuhusu simu janja toleo la 12 Pro Max.

INAYOHUSIANA  Kuna uwezekano wa utumiaji simu gizani kusababisha upofu! #Utafiti #Afya

Muonekano wa simu hiyo umeweza kutoa mwanga wa iwapo simu hiyo itakuwa na urefu wa wastani au la kama ambavyo tunazifahamu rununu mbalimbali zilizopo sokoni/zimeshazinduliwa. Kiujumla rununu hii inafanana na iPhone 5s ingawa si kwa sifa za kiundani.

iPhone 12 Pro Max
Toleo la Pro Max ambalo linafanana na iPhone 5s.

Kwa mantiki hiyo simu hiyo inaaminika kuwa kioo chake kitakuwa na urefu wa inchi 6.7, kamera tatu (3) upande wa nyuma huku mojawapo ikiwa na teknolojia ya LiDAR. Ingawa kwa picha ambazo zimevuja zinaonyesha mpangilio wa muonekano ule wa nyuma bado haujakamilika kwa maana ya kwamba bado inaendelea kuboreshwa.

INAYOHUSIANA  Njia Spesheli kwa Ajili ya Waendesha Baiskeli Kuunganisha Miji kadhaa nchini Ujerumani
iPhone 12 Pro Max
Muonekano wa nyuma kwenye iPhone 12 Pro Max.

Mpaka sasa inaelezwa kuwa muundo wa simu hiyo umekamilika kwa asilimia 70 vikiwa imebaki vipengele vichache kuikamilisha kadri ambavyo itawapendeza wahusika tayari kwa kuzinduliwa baadae mwaka huu na hatimae kuingia sokoni.

Vyanzo: GSMArena, Forbes

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|