fbpx
Afya

Viwanda vya kampuni ya Louis Vuitton kutengeza visafisha mikono

viwanda-vya-kampuni-ya-louis-vuitton-kutengeza-visafisha-mikono
Sambaza

LVMH kampuni inayotengeneza bidhaa za bei za juu (anasa) hii ikiwa ni pamoja na manukato ya Louis Vuitton kutengeneza visafisha mikono kama moja ya kusaidia taifa lao, Ufaransa, dhidi ya gonjwa la Corona.

louis vuittonLVMH ni watengenezaji pia wa vinywaji vya Moët na Hennessy.

Kampuni hiyo inalenga kutumia sehemu ya viwanda vyake vya manukato yake ya Louis Vuitton kutengeneza visafisha mikono (hand sanitizer).

INAYOHUSIANA  EyeQue Check: Kifaa cha kupima macho nyumbani

Kampuni hiyo inategemea kutengeneza kilo 12 ya bidhaa hizo ndani ya wiki moja, na bidhaa hizo zitatolewa bure kwa serikali ya Ufaransa na kwa mahospitali makubwa katika bara la Ulaya.

Nje ya hili kampuni hiyo pia imeagiza zaidi ya maski milioni 40 kutoka kwenye viwanda vya nchini China kwa ajili ya kuisaidia Ufaransa.

Ufaransa ni moja ya taifa lililofanya maamuzi ya kufanya mazuio makubwa ya makusanyiko na shughuli za kibiashara na kusisitiza watu wafanye kazi wakiwa nyumbani. Moja ya sababu ya uamuzi huo ni kutokana na ukosefu mkubwa wa vitu muhimu vya kuwatosha wananchi wote – hasa hasa maski na ‘hand sanitiser’

INAYOHUSIANA  Roboti kutumika kuwahudumia wazee nchini Japani

Je unauchukuliaje uamuzi huu?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |