Mwaka 2001 tarehe 15 mwezi wa kwanza Wikipedia ilizaliwa, kwa sasa ni moja kati ya mitandao inayotembelewa zaidi duniani.
Ikiwa na makala 32,000 za kiswahili mpaka mwezi Januari Kiswahili kinakuwa ni lugha ya 94 kati ya lugha 291, hii ni nafasi juu ikizipita lugha kama kiYoruba na kiZulu.
Wikipedia ndiyo mtandao ulioleta mapinduzi ya upatikanaji wa taarifa, kimsingi katika mtandao huu utapata kila kitu kuhusu chochote unachotaka kujua. Lengo kuu la mtandao huu ni kuhakisha kwamba taarifa mbalimbali zinawafikia watu wengi zaidi.
Wikipedia haijawa na safari nyepesi kwa miaka hiyo kumi na tano, moja ya changamoto ni waandishi wengi wanakata tamaa na kuacha kuandika. Pia bado kuna makala nyingi zinahitaji kuandikwa na bado hazijaandikwa kwa kifupi ni kwamba bado kazi kubwa haijafanyika.
Mwaka 2000 kampuni ya Encyclopedia Britannica ilikua katika kiwango cha juu ikifanya mauzo ya makubwa ya vitabu vyake, miaka kumi na na tano baadaye kampuni hiyo haichapishi tena vitabu vyake na zaidi wasomaji wake wameihama. Wikipedia imefanikiwa kubadilisha namna jinsi watu walivyokuwa wanapata taarifa mbalimbali.
Ingawa watu wengi walidhani Wikipedia haitafika mbali kwa namna ilivyokuwa inaendeshwa (hasa kuwa na wachangiaji wengi) hali kwa sasa imekuwa ni tofauti na hii imejidhihirisha baada ya mtandao huu kuwa ni miongoni mwa mitandao inayotembelewa zaidi.
Wikipedia imejengwa katika ‘application ya wiki’ ambayo inaruhusu watumiaji kusahihisha taarifa kwa urahisi, na hii ndiyo inatajwa kuwa sababu kubwa kwa kukua kwa wikipedia.
No Comment! Be the first one.