fbpx
Intaneti

Idadi ya watumiaji wa Intaneti yaongezeka Ulimwenguni

idadi-ya-watumiaji-wa-intaneti-yaongezeka
Sambaza

Idadi ya watumiaji wa intaneti duniani imezidi kuongezeka na huku bara la Afrika likishika nafasi ya tatu kwa wingi wa watumiaji.

Idadi ya watu wanaotumia intaneti ulimwenguni, kufikia Julai mwaka huu imefikia watu bilioni 4.4, huu ni ukuaji mkubwa kutoka watumiaji bilioni 3 Julai mwaka jana.

kasi ya intaneti tanzania watumiaji wa intaneti
Huduma ya intaneti imekuwa bora zaidi Tanzania kutokana na makampuni mengi zaidi kuzidi kuwekeza. Ila ukubwa wa nchi umekuwa changamoto kuhakikisha maboresho yanafanyika katika kila kona ya nchi

Hayo ni kulingana na taarifa iliyojumuishwa kutoka katika ripoti ya mtandao wa DataReportal iliyochapishwa kuhusiana na idadi ya watumiaji wa Intaneti inayoendelea kuongezeka ulimwenguni.

INAYOHUSIANA  Kuwa Makini Usifukuzwe Kazi Kisa Mitandao Ya Kijamii!

Kanda ya Asia Mashariki ni ya kwanza na watumiaji wa Intaneti wanaofikia bilioni 1, wakati eneo la Asia Mashariki na Asia Kusini likiwa na watumiaji milioni 803.

Idadi ya watumiaji wa intaneti nchi zinazoongoza

China inafuatwa na India ikiwa na watumiaji milioni 560 na Marekani ikiwa na milioni 292. Singapore inafuatiwa na Hong Kong na kisha Korea Kusini.

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi tatu za juu Afrika ambazo idadi ya watumiaji wa intaneti inakua kwa kasi kubwa, hii ikiwa nyuma ya Sahara Magharibi na Djibouti.

INAYOHUSIANA  Netflix Kuwa Juu Zaidi Wakati Amazon Na Disney+ Wakifukuzia!

Tanzania inakadiriwa kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 14.5 kulingana na data za kimataifa.

Bara la Asia kwa ujumla wake lina watumiaji zaidi ya bilioni 2.2, huku bara la Ulaya likifuatia likiwa na watumiaji milioni 719. Bara la Afrika lina watumiaji milioni 525.

Bara la Afrika linaongoza kwa kuwa na intaneti ya kasi ndogo zaidi duniani ingawa kuna wastani wa ukuaji.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.