Baadhi ya mitandao ya simu kama vile Vodacom imeathirika katika eneo la huduma ya intaneti kwa siku ya leo. Baada ya uchunguzi wetu kwa kuwasiliana na baadhi ya vyanzo vyetu vya habari tumepata kufahamu tatizo ni nini hasa.
Inasemekana tatizo lipo kwa upande wa mtoaji mkubwa wa huduma ya intaneti SEACOM. Seacom ni mtandao mkubwa wa waya kubwa za huduma ya intaneti (Fiber) anayeunganisha huduma hiyo ya intaneti kwa Tanzania na mataifa mengine. Inasemekana mitambo yao imekuwa na hitirafu na inashungulikiwa.
Hivyo kama wewe ni mteja wa Vodacom au mtandao mwingine wa simu/huduma na umekuwa unapata shida ya kutumia huduma hiyo basi fahamu hii ndio sababu ya tatizo ilo, na inategemewa mambo yatawekwa sawa.
unajitahidi sana kijana wadau tunafurahi