Wengi wameponda kuhusu ujio wa kipimo janja cha mimba kinachokupatia taarifa kama ni kweli unamimba au hapana kwa kutumia mawasiliano ya bluetooth na app unayoweka kwenye simu yako.
Wengi wanaona teknolojia ya muunganisho wa vifaa na huduma za kiintaneti, ‘internet of things’, inatumiwa hadi pasipo na ulazima ila pia wengine wanaona ni jambo zuri ila tungependa kusikia maoni yako baada ya kusoma zaidi.
Kipimo hichi kinafanyaje kazi?
Kama vile vipimo vingine vya mimba, mwanamke atakojoa na kulowanisha kifimbo spesheli na mkojo na kisha atapata matokeo.
Lakini utofauti ni kwamba katikati ya kukojelea kipimo hicho na kupata majibu kuna taarifa kadhaa zitakuwa zinatumwa kwenye app utakayokuwa umeipakua kwenye simu yako.
Je tunapoelekea tutakua na app kwa ajili ya kila jambo?
App hiyo itakuambia;
>Kama kiwango cha mkojo kilicholowanisha kifimbo hicho spesheli ni kiwango cha kutosha kuweza kupewa majibu
Pia utapata taarifa kama kifimbo hicho spesheli kinafanya kazi kwa usahihi
>Baada ya kulowanisha kipimo (kifimbo) hicho na mkojo kutakuwa na muda wa dakika tatu kabla ya kupewa majibu. Na katikati ya muda huo basi app hiyo itakuwa machaguzi matatu (options),
Educate Me – Ukibofya hapo utapewa elimu mbalimbali zinazohusiana na uzazi
Entertain Me – Utaletewa video mbalimbali za kuburudisha wakati unasubiria matokeo yako
Calm Me – Hapa app hiyo itakuletea miziki ya kiutaratibu ya kukufanya utulie kidogo kama upo katika hali ya hofu
Kitu kikubwa ni kukusaidia kutowaza sana suala la matokeo ya kipimo ulichofanya wakati unasubiria matokeo.
Kama nia yako uliyaichagua kwenye app ya kwamba unataka kupata mimba basi app hiyo itakupa hongera kama kipimo kitaonesha kuna mimba, na kama hakuna utapewa taarifa mbalimbali muhimu za kukusaidia.
No Comment! Be the first one.