Muonekano wa giza unapunguza matumizi ya betri

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Matumizi ya betri kwenye simu janja/vifaa vya kidijiti yanachagizwa kwa kiasi kikubwa na kiasi cha mwanga ambao unakuwa umeweka kitu ambacho kinasabisha kuhitaji kimemeshi ili kuchaji.

Makampumi mbalimbali yanakuja na kipengele ambacho kitaruhusu kuwa na muonekano wa giza kitu ambacho tayari tumeshakiona kwenye Youtube na hata kuwa mbioni kuwekwa kwenye WhatsApp.

Kwa mujibu wa utafiti waliofanya Google na kukiri kuwa muonekano wa giza unasaidia kutunza ubora wa betri na kuongea kuwa ingawa mwanga mkali/mdogo kwenye simu unaathiri matumizi ya betri lakini pia rangi ambayo mtu amechagua kuwepo kwenye uso wa juu pia inachangia kumaliza umeme wa betri.

Kwa vifaa vyenye kioo cha AMOLED kitakuwa msaada zaidi kwenye utunzaji wa betri kwenye muonekano wa giza kulinganisha na bidhaa ambazo zina kioo cha LCD.

matumizi ya betri

Bidhaa zenye kioo cha AMOLED zina uwezo wa teknolojia za kung’ara hata wakati wa giza kitu ambacho kinaweza kisisaidie kwenye vioo vya LCD kwa sababu havina uwezo huo.

Kwenye Youtube kipengele cha muonekano wa giza ndio kinaonyesha dhahiri ni kwa kiasi gani kifaa husika kinatumia betri ikiwa na muonekano wa giza au ule wa kawaida ambao wengi ndio tunaoufahamu.

matumizi ya betri

Kiasi cha mwanga, muonekano wa giza, maatumizi ya brtri kulinganisha mwanga ukiwa mpaka mwisho, muonekano wa kawaida (kwenye Youtube) na kiasi gani cha betri kinachotumika.

Inashauriwa sana kutoweka kiasi cha mwanga mpaka mwisho lakini pia kutotumia rangi za mng’ao ili kufanya betri la kifaa gusika kuweza kudumu na umeme.

Vyanzo: GSMArena, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Apple yathibitisha kuwa inatengeneza magari.
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.