fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple Teknolojia

Fahamu: Apple Waja na MacBook ya Uzito wa Kilo 1!

Fahamu: Apple Waja na MacBook ya Uzito wa Kilo 1!

Spread the love

Baada ya kuendelea kupata mafanikio mengi katika iPhone 6 sasa Apple wakuletea MacBook nyembamba zaidi na yenye uzito mdogo zaidi. MacBook hiyo inayoenda kwa jina la ‘MacBook’, bila ‘Air’ wala ‘Pro’ kama tulivyozoea ina uzito wa kilogramu 0.9 na wembamba wa milimita 13, yaani sentimita 1.3.

MACBOOK_GIGGLES.0.0

Tim Cook akiitambulisha!

Laptop hiyo imetambulishwa kwenye mkutano mdogo uliokuwa umeandaliwa na Apple kwa ajili ya kuonesha mambo mengi yanayoweza fanyika kwa kutumia saa yao mpya. 

Sifa kuu za laptop hii ni kama ifuatavyo;

i. Kwa wembamba wa sentimita 1.3 imeifanya MacBook hii kuwa nyembamba kwa zaidi ya asilimia 25% ukilinganisha na toleo jembamba la MacBook Air.

macbook-tanzania-3

ii. Inakioo cha upana wa inchi 12 pia kikiwa na kiwango bora cha muonekano wa Retina na ‘resolution’ ya 2304 x 1440. Apple wanadai kioo hichi kinakula chaji kidogo sana kwa zaidi ya asilimia 30% kikilanganishwa na vioo vinavyotumika kwa sasa.

iii. Mfumo wa CPU unaoiendesha umeondoa ulazima wa kuwa na feni ya kuondoa joto, hivyo usitegemee kelele za feni wala joto sana kwani imetumia teknolojia mpya ya CPU kutoka Intel inayoenda kwa jina la Core M Broadwell CPU. Tazama picha china inayoonesha tofauti ya CPU hii na zile zinazotumika kwa sasa, CPU mpya ni ndogo kwa takribani asilimia 67%.

Ya juu ni bodi ya CPU iliyokwenye MacBook hii mpya na chini ni bodi ya CPU  iliyokwenye MacBook za sasa.

Ya juu ni bodi ya CPU iliyokwenye MacBook hii mpya na chini ni bodi ya CPU iliyokwenye MacBook za sasa.

iv. Pia kuna teknolojia mpya wameitumia katika kibodi zake ambazo wenyewe wanadai ni bora zaidi na imepunguza ata ukubwa mzima wa kibodi katika laptop hiyo.

Kibodi za MacBook hii mpya

Kibodi za MacBook hii mpya

v. Itakuwa na RAM ya GB 8 na pia uwezo wa betri wa zaidi ya asilimia 34 ukilinganishwa na MacBook za sasa.

SOMA PIA  Toleo jipya la Nokia 5310 Xpress Music

vi. Kutakuwa na matoleo mawili, kuna moja la dola 1,299 za kimarekani (Milioni 2.37 za Kitanzania) ina prosesa 1.1 Ghz Core M, na yenye ukubwa wa diski uhifadhi wa GB 256 katika teknolojia ya SSD.  Toleo jingine ni la  dola 1,599 za kimarekani (Milioni 2.9 za Kitanzania)  ina prosesa 1.2 Ghz na ukubwa wa diski uhifadhi wa GB 512 (SSD).

SOMA PIA  Zijue Laptop Zinazoendeshwa Na 'Google Chrome OS' Maarufu Kama Chromebook!

[metaslider id=2801]

Itegemee MacBook hii sokoni ifikapo mwezi wa nne mwaka huu. Kumbuka unaweza kuwasiliana nasi kupitia mhariri (at) teknokona.com au kupitia akaunti zetu za Twitter, Facebook na Instagram .

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania