Je wewe utaweza kuvaa saa ya zaidi ya dola 10,000 za kimarekani? Basi Apple wanafikiri usipoweza nunua hiyo basi utaweza kununua angalau ya bei ya chini kabisa ambayo ni dola 350 ambazo ni takribani Tsh laki 6 na nusu.
Apple wametambulisha saa ambazo zitaanza kupatikana Marekani na baadae duniani kote kuanzia mwezi wa nne. Saa hizo zinazopatikana katika aina zaidi ya 38 zimegawanyika katika makundi mbalimbali.
Kutakuwa na zilizotengenezwa kutumia madini ya fedha, chuma (steel), alumini na dhahabu., bei zitategemea itaanzia laki sita na nusu hadi dola 18,000 za Marekani (Tsh Milioni 33). Upo hapo?
Ukitaka kumiliki simu ya iWatch, Apple Watch ya kiwango cha dhahabu basi itakubidi utumie kati ya milioni 18 hadi 33 kutegemea na chagua lako.
Kumbuka kutakuwa na aina zaidi ya 30, sababu ya kuja na aina nyingi sana za simu hiyo kwa kiwango na ubunifu tofauti tofauti wamedai ni kwamba kwa sababu wanatambua watu wasingefurahi kukaa sehemu moja wakiwa wamevaa saa za kufanana.
-Apple Watch 38mm $549 hadi $1049, Apple Watch 42mm $599 hadi $1099
–Apple Watch Sport $349 hadi $399
-Apple Watch Edition – Kuanzia $10,000
*$ = Dola za kimarekani
Je saa hizi ni kama ulizozizoea?
Hapana, kumbuka hizi ni saa janja!
Sifa zake;
– Inatumia toleo spesheli la iOS na hivyo kuna apps spesheli zinazotengezwa kwa ajili ya kuweza kutumika kwenye saa hizo. Apple wamesema hadi sasa tayari kuna apps si chini ya elfu moja na zilizopo ni pamoja na Facebook, WeChat, na Instagram.
– Kuondoa kakibodi mguso (touch) kadogo kalikopo kwenye saa hiyo bado utaweza kuandika ujumbe na kufanya mengine mengi kwa kuiongelea kupitia programu ya Siri.
– Utaweza kuona taarifa fupi (notifications) zilizojitokeza kwenye simu yako ya iOS bila kugusa simu. Na pia kupitia saa hizo utaweza kubofya na kuondoa taarifa hizo.
Vipi kuhusu chaji?
-Cha ajabu sana ingawa bei ya saa hizi ni ghari sana, CEO wa Apple, Bwana Cook alikiri ya kwamba kwa utumiaji wa kawaida tuu itambidi mtu aichaji saa yake karibia kila siku.
Tazama Picha Zaidi Hapa Chini;
[metaslider id=2814]
No Comment! Be the first one.