fbpx

Nokia X7: Simu nyingine kutoka Nokia

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Nokia wametoa simu janja (rununu) kadha wa kadha mwaka 2018 na kwa juhudi hizo wanaendelea kujirudisha kwenye nafasi nzuri ya kiushindani kwani safari hii wamekuja na Nokia X7.

Nikikuuliza ni rununu ipi unayoipenda zaidi kutoka Nokia si ajabu ukanitajia simu janja zaidi ya moja ambazo unavutiwa nazo kwa namna moja au nyingine lakini hapo sio mwisho wa wewe kuvutiwa na bidhaa za Nokia hasa kwa upande wa simu janja. Sasa Nokia X7 ina sifa zifuatazo:-

Kipengele

Nokia X7

Kioo Kioo kina urefu wa inchi 6.18  Full HD LCD (1080+ pixels)
Muonekamo Ina umbo la herufi “V” na inafanana kama Nokia 7.1 Plus
Kipuri mama Snapdragon 710 ndio iliyowekwa ikiwa ni toleo la karibuni kabisa
Nokia X7

Simu iliyokama toleo la Nokia 7.1 kumbe ni Nokia X7.

Kipengele

Nokia X7

Kamera Nyuma: Kamera mbili-MP 12 na MP 13, kama kawaida zikiwa zimetengenezwa na Zeiss.

Mbele: Ina kamera moja yenye MP 20

RAM/Diski uhifadhi
  • 4GB RAM kwa GB 64 memori ya ndani,
  • 6GB RAM kwa 64GB memori ya ndani na
  • 6 GB RAM kwa 128GB memori ya ndani
Betri
  • 3500 mAh ndio nguvu ya betri na haliwezi kutoka
  • Pia ikiwa na teknolojia ya kuchaji haraka; ndani  ya dakika 30 simu inakuwa imeshajaa chaji
Nokia X7

Ubora wa picha ambao unatokana na MP 12-13MP/kamera ya mbele yenye MP 20.

Kipengele

Nokia X7

Bei

$245|Tsh. 563,500 (4/64GB), $290|Tsh. 667,000 (6/64GB) na $360|Tsh. 828,000 (6/128GB)

Rangi

Nyeusi, Nyekundu, Bluu mpauko na Fedha

Mengineyo

  • Inatumia kadi mbili za simu kiwango cha GSM / CDMA / HSPA / LTE,
  • Ina Android 8.1 (masasisho ya Android 9 Pie ni mpaka hapo baadae),
  • Ina sehemu ya kuchoka spika za masikioni,
  • Ulinzi wa kutumia alama ya kidole upo kwa nyuma.
INAYOHUSIANA  Simu janja: Zifahamu Oppo A9 na A9x

Kwa taarifa tu simu janja husika bado haijaingia sokoni lakini mtu anaweza akaagiza na mara tu itakapoingia sokoni itatumwa.

Vyanzo: GSMArena, Trusted Review, India Today

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.