fbpx

Tafuta Mtu Yeyote Mwenye Simu kwa Njia Hizi

1

Sambaza

Zipo sababu nyingi za kutafuta mtu zikiwemo undugu (kama mtoto wako) na unataka usalama wake. Labda mko safarini, labda ni marafiki na mnataka usalama kati yenu. Pengine pia, una sababu zako za kiuchunguzi zaidi na unataka umfuatilie mtu unayemjua au usiyemjua au labda pengine umepoteza au umeibiwa simu na unataka kuitafuta.

Teknolojia ya sasa inafanya mambo yote haya yawe marahisi zaidi kwani kuwepo kwa mfumo wa GPS, tekniki ya ‘triangulation’ (inayotumia minara ya simu) na maeneo ya wayalesi kunafanya kuweka simu kwenye ramani kirahisi.

Fanya yafuatayo kutafuta simu yoyote kwenye ramani ya dunia.

1. Sajili Simu yako/ya mtu Vizuri

.Simu za kisasa, yani simu-janja huja moja-kwa-moja na mfumo utakao kusaidia kujisajili, punde tu utakapoiwasha.

Kusajili simu vizuri ni hatua ya kwanza kabisa katika kuiwezesha kutafutika kwenye ramani na pia kuilinda simu yako. Simu za kisasa, yani simu-janja huja moja-kwa-moja na mfumo utakao kusaidia kujisajili, punde tu utakapoiwasha. Hii ni kama umeinunua mpya. Vyovyote ulivyopata simu hiyo, unahitaji kuisajili kwa kutumia barua-pepe yako. Kwa simu za zamani kidogo, inabidi uiwezeshe kwa kujisajili na huduma ya GPS kwa makampuni ya mambo hayo ambayo yako machache hapa Tanzania. Huduma ya GPS inaweza pia kuwekwa kwenye gari au mali yoyote inayoweza kuhamishwa, hata saa ya mkononi. Cha muhimu hapa ni kujua kwamba kama unataka kufuatilia simu, itakupasa uisajili kwanza na huduma sahihi.

2. Tumia programu kufuatilia Mwizi/ Simu iliyopotea:

Unaweza kuifuatilia simu kwenye ramani kwa GPS na app iwapo tu ulipakia app hiyo kwenye simu hiyo

Unaweza kuifuatilia simu kwenye ramani kwa GPS na app iwapo tu ulipakia app hiyo kwenye simu hiyo

Kama unatumia simu ya kawaida (isiyo simu-janja) utatumia programu ulizopewa na kampuni ya huduma ya GPS. Kama ni simu-janja, basi kuna uwanja mkubwa zaidi wa kucheza. Zipo programu nyingi za kufuatila simu za aina hizo kutegemea na nini unataka kufanya.

INAYOHUSIANA  Vodacom Tanzania wana huduma mpya

Android

iPhone

Windows phone

Android Device Manager : App ya msingi kutoka Google kwa ajili ya kutafuta simu yako. Programu hii Inafaa kama umeruhusu simu yako kufuatiliwa na Google. Find My iPhone + iCloud: App ya msingi kwa vifaa vya Apple kwa kutafuta simu na kufuta taarifa zako, pale zinapoibiwa. Find My Phone: Chaguzo ya Windows inayotumia minara ya simu kutafuta simu yako.
Where’s My Droid, Plan B, Android Lost Free, Prey: App kama hizi zina uwezo tofauti na unaweza kujaribu kuona ipi inakufaa. GadgetTrak, Mobile Spy, Device Locator: App mbadala kwa simu za Apple

App kama hizi za kufuatilia zina uwezo wa:

  • Kuzima na kuwasha GPS, -intaneti, wayalesi, mlio wa simu,
  • Kukutumia namba za watu waliopigiwa/waliopiga simu
  • Kupiga picha sehemu simu ilipo kufuta taarifa zako.

3. Fuatilia ndugu na marafiki

Kama umekubaliana na nduguye, mpenziwe au rafiki kufuatiliana kwa sababu mbalimbali ikiwemo usalama, basi hamna budi wote muwe na programu flani ya kushirikishana ramani zenu kwa mtandao. Programu kama hizi na za kuaminika ni kama Find My Friends, Life 360, Phone Tracker, TopSpyApp, Connect, Mama Bear, My Mobile Watchdog na Time Away. Programu hizi zina uwezo wa kumtaarifu mtu uko wapi, umefika nyumbani au kazini au shuleni au kama umeondoka eneo ambalo mmekubaliana kuweka mpaka msivuke na kutoroka na pia ina uwezo wa kutuma namba zilizopigwa/ kupokewa na app ambazo muhusika ametumia au hata tovuti alizotembelea. Huduma kama hizi zinawafaa wazazi wanaotaka kuwapa uhuru watoto wao lakini chini ya ulinzi.

INAYOHUSIANA  Samsung Galaxy Fold: Simu ya kwanza ya display/kioo cha mkunjo kutoka Samsung

Mbali na app kama hizo, mnaweza pia kutumia vipengele vya app za mawasiliano kama viber na facebook messenger zinazoambatanisha taarifa za eneo pamoja na ujumbe.

4. Tumia App kufuatilia Kiuchunguzi

Kama wewe si serikali au jasusi (ambao wana zana za kila aina) na unataka kumchunguza mtu, hakuna ujanja zaidi ya kufanya tukio la aina yake na kuweka kifaa cha GPS kwenye simu husika au kuweka app mojawapo ya kufuatilia kati ya zilizotajwa hapo juu na kuificha app hiyo kwa app nyingine kama ‘poof!’ Itakubidi ufanye hivyo wakati mwenzio amelala au labda ametoka bila kuchukua simu au umeiteka hiyo simu.

5. Tafuta mtu Aliyekupigia

Kuna app kadhaa zinazodai kwamba zina uwezo wa kukupa eneo la mtu aliyekupigia (Kama CIA – Caller Identification App ya android, Caller ID App, na WhosCall) lakini ukweli ni kwamba bado teknolojia ina mipaka ikifika kwenye suala hili nyeti. Bado kwenye nchi nyingi sheria haijaruhusu simu kutangaza eneo la mtu bila ruhusa yake. Hatahivyo, hadi sasa zipo njia kadhaa za kutambua jina la anayekupigia bila ya taarifa kamili za eneo lake kama kutumia huduma za pesa(m-pesa, tigo-pesa, n.k.), app kama true caller na app ya messenger ya facebook.

INAYOHUSIANA  Uwezo wa betri/Kipuri mama - Samsung Galaxy S10 Lite

Vyanzo:

tomsguidemakeuseof

Picha Na:

c4learn.com, gizmag.com, techpp.com

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

1 Comment

Leave A Reply