fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta Teknolojia

Windows 10 Haitakuwa Bure kwa Wote Tena!

Windows 10 Haitakuwa Bure kwa Wote Tena!

Spread the love

Kila baada ya siku chache siku hizi lazima kuwe na habari inayohusu toleo lijalo la programu endeshaji kutoka Microsoft, Windows 10. Katika hali inayoonekana si ya kawaida kupitia afisa mwingine wa kampuni hiyo wametoa taarifa inayopingana na walichosema mapema mwaka huu ya kwamba watu wote wenye programu endeshaji ya Windows wataweza kupata toleo hilo jipya bure kupitia kusasisha (update/upgrade) kwenye intaneti.

Soma – “Windows 10 Itapatikana ‘bure’ Kwa Mwaka Mmoja!

Walisema hii itakuwa kwa watumiaji wote waliopata Windows kwenye njia rasmi na ata wale ambao wamepata za kiwizi, sasa wamebadilika. Wamesema uwezo wa kupata toleo hilo bure katika kipindi cha mwaka wa kwanza utakuwa kwa watumiaji wa matoleo rasmi tuu, yaliyopatikana kihalali.Muonekano Unaotarajiwa wa Windows 9

SOMA PIA  Bidhaa Mbaya Ambazo Zimeshawahi Kutengenezwa Na Makampuni Makubwa Ya Teknolojia!

Bwana Terry Myerson wa Microsoft aliandika kwenye blogu rasmi ya kampuni hiyo, akitoa taarifa ambayo wengi walikuwa bado hawajaiamini vizuri kama kweli Microsoft wangeruhusu hadi watu wanaotumia Windows 7 na 8 walizozipata kwenye mitandao kama ya Torrent wataweza kusasisha kompyuta zao kwenda Windows 10. Juzi juzi kampuni hiyo imetoa orodha rasmi ya matoleo ya Windows 10, unaweza kusoma zaidi hapa – Fahamu Matoleo Rasmi ya Windows 10, katika matoleo hayo ni Windows 10 Home, Windows 10 Mobile na Windows 10 Pro ndio yatapatikana bure katika kipindi cha mwaka mmoja kwa wateja wake wa sasa.

Hivyo kama unatumia toleo la Windows la wizi fahamu kutakuwa na njia mbili za wewe kupata toleo la Windows 10; ya kwanza ni kupitia kulipia, wamesema watawapa uwezo wa kulipia mtandaoni na hivyo kuweza kupata toleo la Windows 10 kupitia kusasisha (Update/Upgrade), njia ya pili itabidi utafute za wizi tena. Ila inavyoonekana kupata lililo rasmi ndio utakuwa uamuzi mzuri zaidi kwani hii ndio mara ya mwisho utalipia, kwani kuanzia sasa watakuwa wanasasisha (update) tuu, hakutakuwa na Windows 11 n.k, soma –Baada ya Windows 10 Usitegemee Kuona Windows 11

SOMA PIA  Simu Janja 'Phantom 9' Kutoka TECNO Hii Hapa!

Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia ktk kiswahili, kumbuka kusambaza makali kwa marafiki. 👍

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania