Zamani sana ilikuwa vigumu sana kufanya lolote kubwa zaidi ya kusoma na kuprinti pale utakapopata faili lililo kwenye mfumo wa PDF. Kama ungetaka kuandika au kufanya mabadiliko yeyote makubwa kwenye faili husika basi ingekubidi umiliki programu ya Adobe Pro. Na programu hii ni ya kununua, na kwei bei ya juu.
Leo tutakuonesha njia fupi ya kuweza kufungua na kufanya mabadiliko kama vile kuandika au kujaza fomu kwa faili la PDF kutumia programu ya Microsoft Word kuanzia toleo la mwaka 2013 na kuendelea.
1. Fungua programu ya Microsoft Word, kisha bofya eneo la ‘Open Other Documents‘
2. Nenda hadi lilipo faili hilo la PDF, kisha lichague
3. Programu ya MS Word itaanza kulibadilisha faili hilo kwenda mfumo wa Word ili kukuwezesha kulitumia. Kuwa mvumilivu kwani kulingana na ukubwa wa faili hilo na uwezo wa kompyuta yako tukio hili linaweza chukua muda kidogo
4. Baada ya faili lako kufunguka kumbuka kubofya eneo la ‘Enable Editing’, kufanya hivi kutakupa uwezo wa wewe kuweza kuandika na mabadiliko mengine
5. Ukiona kaujumbe kama haka chini bofya kukubali, yaani ‘Yes’
6. Sasa utaweza fanya mabadiliko yeyote uyapendayo na kisha ukimaliza unaweza kuprinti au kuhifadhi (Save) kwenye mfumo wa PDF tena au kwenye mfumo wa Word.
Kumbuka kusambaza ujanja huu kwa wengine piaaaa! Kumbuka unaweza kuwasiliana nasi kupitia mhariri (at) teknokona.com au kupitia akaunti zetu za Twitter, Facebook na Instagram .
No Comment! Be the first one.