Kwa kipindi kirefu kampuni ya Apple ilikuwa imeshikilia msimamo wa kutoamini kuhusu simu au tableti zilizokubwa lakini kupitia iPhone 6 na iPhone 6 Plus tuliona msimamo huo ukiondoka na watafiti wengi wamechukulia mabadiliko hayo yamesukumwa na mafanikio ya simu na tableti za Android ambazo zinakuja kwa ukubwa mbalimbali na zinafanikiwa.
Sasa Apple kuja na iPad Pro hivi karibuni, taarifa hizi hazijathibitishwa na kampuni hiyo ila vyanzo mbalimbali vya habari na pamoja na kuibuka kwa picha kutoka kiwanda kinachotumiwa na Apple huko China kuonesha iPad hizi kuwa tayari zimeanza kutengenezwa.
Kampuni ya Apple imekuwa inajitahidi kufanya usiri mkubwa wa shughuli zao hivyo hawakutegemewa kukubali au kukata kuhusu ujio wa iPad Pro (Wengine wana wasiwasi jina linaweza likawa iPad Plus au iPad Pro Plus 🙂 )
Je inasifa gani?
- Kioo inchi 12.2 – 12.9
- Uzito gramu 437
- RAM GB 2
- ‘Wireless’ & 3G /4G
- Kuchaji bila waya (Wireless charging)
- Diski Uhifadhi GB16 , GB32, GB64 au GB128
Pia kuna uwezokano wa teknolojia ya 3D inayofahamika kwa jina la Stylus inategemewa katika toleo hili. Apple kufanya uamuzi huo hakita kuwa kibaya kwani kuna umuhimu wa kufanya bidhaa zao zote ziwe na majina ya kufanana ili kutochanganya wateja. Kumbuka laptop kutoka Apple zinakuja kwa majina mawili tuu, MacBook Air na MacBook Pro, uamuzi huu unaonesha wataka iPad pia ziwe zinatoka kwenye familia za majina hayo pia.
Kumbuka tutaendelea kufuatilia habari hii na mabadiliko na mengine mapya tutayaweka hapa!
Je wewe ni mpenzi wa bidhaa za Apple. Soma habari mbalimbali kuhusu Apple kwa kubofya hapa -> Makala kuhusu Apple
Pia unaweza soma kuhusu apps za iPhones na iPad maarufu zaidi kwa mwaka 2014 HAPA!
No Comment! Be the first one.