fbpx

Kompyuta, Teknolojia

Toshiba yajiondoa kwenye biashara ya kompyuta

toshiba-yajiondoa-kwenye-biashara-ya-kompyuta

Sambaza

Dunia nzima inafahamu kuhusu kompyuta za Toshiba ambazo wamekuwa kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya robo karne sasa na wamefanikiwa kutengeneza, kuuza aina mbalimbali vipakatalishi ulimwenguni kote.

Si suala la kupinga kuwa Toshiba imekuwa ikitengeneza kompyuta nzuri za ubora kulingana na ukuaji w teknolojia lakini sasa wameamua kujiweka pemebeni na biashara hiyo kwa asilimia 100. Miaka miwili iliyopita, Toshiba iliuza 80.1% ya hisa (sawa na $36 milioni) zake kwa Sharp na Juni mwaka huu kampuni hiyo hiyo ikamalizia kununua 19.1% za hisa zilizokuwa zimebaki. HIvyo basi, Sharp inamiliki kwa asilimia zote Toshiba na hivi sasa kitengo hicho cha kutengeneza kompyuta kinaitwa  Dynabook.

Historia yake kwa ufupi sana

>Toshiba ilitengeneza kompyuta (kipakatalishi) yake ya kwanza miaka thelathini na mitano iliyopita (35) iliyoitwa The T1100 na haikuingizwa sokoni mara moja kutokana na viongozi wake wakuu kutokuwa na uhakika lakini baadae ilikuja kuingia sokoni na kuuzwa karibu $2,000.

>Kati ya miaka ya 90 na 2000, Toshiba ilikuwa ni moja ya kampuni ambayo yalikuwa kwenye umaarufu wake kwenye biashara ya utengenezaji wa komyuta lakini kadri washindani walivyozidi kuongezeka wakaanza kutetereka kimauzo. Takwimu zinaonyesha mauzo ya komyua za Toshiba milioni 17.7 mwaka 2011 hadi miloni 1.4 mwaka 2017.

Kwenye biashara
Muonekano wa kipakatalishi cha kwanza kilichotengenezwa na Toshiba T1100.

Hao ndio Toshiba ambao wameamua kujiweka kando na kuwaachia wengine waendeleze gurudumu la biashara ya kompyuta. Wewe ni mpenzi wa vipakatalishi vya Toshiba? Tuambie umeipokeaje habari hii?.

Vyanzo: The Verge, Business Standard

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|