fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

simu Teknolojia

Uchambuzi wa Oppo A31, uwezo na sifa

Uchambuzi wa Oppo A31, uwezo na sifa

tecno

Kampuni ya Oppo ni kampuni toka nchini Uchina inayokuja kwa namna nzuri katika nyanja ya simu janja duniani.

Simu hii ya Oppo A31 ni moja kati ya matoleo yao ya kiwnago cha kati yenye thamani nzuri na ujazo wa sifa mbalimbali zenye kufanikisha matumizi mazuri ya simu.

Oppo A31

Oppo A31

Baadhi ya sifa hizo ni:

  • Kioo (Display) cha teknolojia ya LCD chenye ukubwa wa inch 6.5,
  • MfumoEndeshi (OS) wa Android 9,
  • Chipset ya Mediatek Helio P35,
  • 64GB 4GB RAM, 128GB 4GB RAM, 128GB 6GB RAM,
  • Mfumo wa kamera tatu nyuma (MP 12, 2 na 2) na kamera ya MP 8 mbele,
  • Betri yenye uwezo wa 4230 mAh.
SOMA PIA  Ondoa programu ya QuickTime kwenye kompyuta yako! #Usalama

Simu hii ina teknolojia ya utambuzi wa alama za vidole (Fingerprint). Pia, inasapoti teknolojia ya mawasiliano ya 4G kwa ajili ya mtandao wenye kasi. Simu hii ina teknolojia za WiFi na Bluetooth bila kusahau huduma ya FM Radio.

tecno

Oppo A31

Kamera 3 amabzo zina uwezo wa kuvuta kitu kwa karibu zaidi.

Simu hii pia ina sehemu ya kuchomeka waya wa chaji aina ya microUSB 2.0, pia ikiwa na sehemu ya kuchomeka waya ya earphones. Matoleo ya rangi kwa simu hii ni matatu, Nyeupe, Nyeusi na Kijani.

SOMA PIA  Project Fi: Mtandao Mpya wa Simu kutoka Google. #Teknolojia

Kiujumla bei yake inahimilika inayoanzia $355|zaidi Tsh. 816,500 kwa bei ya ughaibuni lakini pia rununu hii ipo sokoni kwa muda mrefu tangu itoke.

Vyanzo: GSMArena, Gadgets 360

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania