fbpx

Teknolojia

Bustani ya kidigitali yenye sauti mbalimbali za matunda yaundwa #Teknolojia

bustani-ya-kidigitali-yenye-sauti-mbalimbali-za-matunda-yaundwa-teknolojia

Sambaza

Uimbaji wa nyimbo mbalimbali wakati mtu anapofanya kazi ngumu mathalani bustanini/shambani kwa karne imekuwa kama motisha ya kumfanya mtu aweze kuendelea na kazi yake bila kuhisi kuchoka kwa muda mrefu tu ila kwa mapinduzi ya teknolojia hivi sasa kuna bustani janja yenye sauti nzuri.

Kwa karne zinavyozidi kwenda ndio teknolojia nayo inavyozidi kwenda mbali zaidi kwa watu kuweka fikra na mawazo yao na kuja na vitu vipya kwa ajili ya manufaa ya wengi kwa ujumla. Ulishawahi kusikia kuhusu bustani ya kidigitali?! Ndio, bustani hiyo ipo na hivi karibuni imewekwa kwenye maonyesho huko Tokyo, Japani.

SOMA PIA  QIK: App Mpya Ya Video Kutoka Skype!
Bustani ya kidigiti iliyoundwa kwenye mahabara ijulikanayo kama PARTY.

Yote kuhusu bustani ya kidigitali iliyopendezeshwa na teknolojia.

Bustani ipo katikati ya jiji la Tokyo ambayo imetokea kuwavutia wengi kutokana na kile ambacho mbunifu wake, Bw. Ray Kunimoto amekifanya kwenye bustani hiyo ya kijanja ambayo inavutia sana. Bustani hii inapendezeshwa na taa na sauti mbalimbali ambazo zinazunguka bustani nzima (kama kilimo cha greenhouse).

Kwa kugusa tu mmea fulani basi itatoka sauti ya mmea husika mathani pale sauti inayotokana na kucuma chugwa mtini huku taa zenye rangi mbalimbali zikienda pamoja na mlio kutokana na mmea ambao mtu ameushika.

Bustani ya kidigiti: Mtalii anatakiwa kulishika jani kwa upole mara 3 kuweza kufurahia sauti ya kwenye mmea alioushika

Sauti ambazo zinatoka baada ya mmea fulani kuguswa zinatokana na kurekodiwa kwa sauti halisi ya pale mtu anapokwenda shambani kuchuma tunda/mboga za majani, sauti inayotokana na kutafuna kitu mdomoni, sauti inayotokana na kugusanisha majani/kusugua mbegu na kisha kompyuta kutumia kutengeneza melody saba.

Kila mmea ambao utashikwa utatoa sauti ya aina yake bila kujirudia zikiwemo sauti mbalimbali za ala za muziki mfano tarumbeta.

Bustani ya kidigiti: Muonekamo wa mbali wa bustani ya kidigitali.

Mpaka hivi sasa bustani hiyo imetokeea kuwavutia wati mbalimbali wanaotembelea eneo hilo na kuweza kujionea uzuri wa bustani ya kidigitali ambayo itaendelea kuonyeshwa mpaka Novemba 5 2017. Je, unaizungumziaje bustani hii ya kidigitali?

Vyanzo: Colossal, Engadget

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|