Wakati Apple wanazindua bidhaa zao mwezi wa Septemba kama iliyo kawaida yao kuna vitu kama AirPods 3, kompyuta za MacBook Pro hazikutambulishwa na ilikuwa imetegemewa hivyo.
Septemba 14 mwaka huu Apple walizindua iPhone 13, 13 Pro, 13 Pro Max halikadhalika Watch series 7, iPad, iPad Mini na ingawa bado hazijaanza kuuzwa lakini habari zake zinasomwa kwa wingi mitandaoni.
Sasa pamekuwepo panda shuka kuhusianna na ujio wa AirPod 3 lakini pia kompyuta aina ya MacBook Pro ambazo utengenezaji wake unaendelea na zitazinduliwa mwaka huu. Kompyuta za Apple toleo la MacBook Pro zinaelezwa kuwa na zinaelezwa kuwa na kioo chenye ukubwa wa inchi 14 na nyingine 16; zinakuwa ndio kompyuta za kwanza za Apple kioo chake kuwa cha ung’avu wa hali ya juu (mini LED).

Mwakani je?
Mwaka 2022, Apple wanatazamia kutoa toleo jingine la spika za masikioni ambazo ni AirPods Pro 2 ambapo pia inatazamiwa iPad Pro zitatoka pia. Tabiti hizo zinaelezwa kuwa za kioo kwa upande wa nyuma lakini pia kuwa na teknolojia ya kuchaji bila kutumia waya hivyo MagSafe itatumika kufanya kazi hiyo halikadhalika kutumia tabiti kuchaji AirPods.
Yapo mengi ambayo ni ya “Chini ya kapeti” ila kama kawaida yetu tukusihi kuendelea kutufuatilia na tutawahabarisha kila inapoitwa leo kwani hii ndio kazi yetu na tunaipenda.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.