Nokia Mobile kutambulisha simu mpya mwezi wa Oktoba. Kampuni ya HMD Global inaendelea na utengenezaji wa simu za Nokia, na Oktoba 6 tutegemee vitu vipya kutoka kwao.
HMD Global hawajatangaza vifaa vyote vitakazotangazwa ila tayari habari za chini chini zinasema kutakuwa na utambulisho wa simu janja ya Nokia G50 5G, na tableti ya Nokia T20. Hii itakuwa ni tableti ya kwanza kutoka ikibeba jina la Nokia tokea mara ya mwisho mwaka 2015 ilipotambulishwa Nokia N1 Slate.
Taarifa ya tukio la utambulisho wa vitu vipya vinavyobeba chapa ya Nokia uliwekwa wazi pia na kampuni ya Nokia kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
Our family keeps growing.
Coming 6.10.21 pic.twitter.com/B55fUMWAOs— Nokia Mobile (@NokiaMobile) September 20, 2021
Kuhusu Nokia G50 5G
- Itakuwa simu janja inayokuja na teknolojia ya 5G.
- Prosesa ya Qualcomm Snapdragon 480
- Display ya ukubwa wa inchi 6.8 HD+
- Kamera: Mfumo wa kamera tatu (macho matatu), kuu ikiwa ni ya Megapixel 48.850
- Betri la mAh 4000
Kuhusu tabiti ya T20
Vyanzo mbalimbali vinategemea pia Nokia kutambulisha tableti ya T20 inayotumia programu endeshaji ya Android.
Display – inchi 10.36. RAM ya GB 4 huku ikiwa na diski uhifadhi wa GB 64.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinasema tableti hiyo itakuja ikiwa inatumia Android 11 na prosesa ya Unisoc.
HMD Global ni kampuni ya nchini Finland yenye hakimiliki ya utengenezaji na uuzaji wa simu zinazotumia jina la Nokia. Kupitia makubaliano yao na kampuni ya Nokia – ya zamani, iliyojitoa kwenye biashara ya utengenezaji na simu na kubaki kwenye miundombinu na huduma za sekta ya mawasiliano, HMD Global wameendelea kuleta simu zinazobeba jina la Nokia.
Shirika la Nokia pia ni wawekezaji katika kampuni ya HMD Global na wanatoa ushirikiano wa kiteknolojia katika bidhaa zote zinazobeba jina hilo.
No Comment! Be the first one.