fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps iOS Teknolojia

Clubhouse inaboreshwa kuweza kualika watu wengi

Clubhouse inaboreshwa kuweza kualika watu wengi

Spread the love

Clubhouse inaboreshwa ambapo ni programu tumishi ambayo inaendelea kupata watumiaji wengi duniani kote ambapo siku hadi siku inaendelea kuboreshwa kutanua wigo lakini kuifanya izidi kuvutia.

Programu hii tumishi ilikuwa ikipatikana kwa wanaotumia iOS lakini baadae wahusika wakaamua kuipeleka kwenye Android ambapo kimsingi hatua hiyo imeongeza watumiaji wake. Kwa wasiofahamu Clubhouse ni programu tumishi ambayo ndani yake mtu anaweza akaendesha mahojiano mubashara na watu wakaingia ndani ya vyumba maalum kuweza kusikiliza kinachozungumzwa huko.

Clubhouse inaboreshwa

Clubhouse inaboreshwa: Ndani ya Clubhouse kuna vtumba ambavyo anayealikwa basi anaingia huko kuweza kusikiliza mahojiano/mazungumzo mubashara watu na maarufu kama Mark Zuckerberg, Elon Musk kuweza kuongea na watu wao.

Sasa kuna maboresho ambayo yanafanyika kwenye programu tumishi husika ambapo kuna kitufe kipya kiitwacho “Wave” kinatengenezwa kinacholenga kuwapa uhuru watumiaji wa Clubhouse kualika watu kuja kuingia ndani na kusikiza kile ambacho kinaendelea huko.

Kitufe hiki ambacho kinatengenezwa kitawekwa kwenye ukurasa wa wasifu (profile) ambapo mtu akibonyeza wewe unapata taarifa kuwa mtu anataka kuongea na wewe kwa njia ya maandishi na mtu ataruhusiwa kuingia kwenye chumba iwapo tu utakubali ombi.

Maboresho hayo yanalenga watu kuanza tuu kukutumia ujumbe hivyo kitufe hiki kitasaidia watu kuweza kuchuja nani wa kumruhusu kuzungumza nae au kutojibu kitu. Kuhusu ni lini bado kipengele hiki hakijaanza kupatikana kwa wote na kutegemewa kuja siku zijazo.

Vyanzo: Engadget, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania