WhatsApp ni moja kati ya mitandao ya kijamii maarufu unaomilikiwa na kampuni ya Meta, Kwa sasa ipo kwenye muendelezo wa ubunifu ili kumuwezesha mtumiaji kuweza kuweka ujumbe wa sauti sehemu ya WhatsApp Status. Haya ni mabadiliko yatakayomuwezesha mtumiaji kurekodi sauti na kuweka kwenye sehemu yake ya status ambapo kabla ya teknolojia hii eneo hili la status lilikuwa linaruhusu kuweka video isiyozidi sekunde thelathini na picha pekee.
Dunia kwa sasa inapitia mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia hivyo basi ili kuendana na kasi ya mabadiliko hayo WhatsApp wamemeamua kutanua zadi mipaka yake na kuwarahisishia na kuwaongezea machaguo mengi zaidi watumiaji wake. Huduma hii itakuwa inapatikana kwenye toleo jipya kabisa la WhatsApp ambalo ni 2.22.16.3; na kwa sasa linatumika kama sehemu ya majaribio kwa watumiaji wa Android pekee.
Hadi sasa WhatsApp haijatangaza rasmi ni lini toleo hilo jipya litaanza kutumika rasmi na watumiaji wake lakini pia hawajaweka wazi majaribio kwa watumiaji wa IOS. Kwa maendeleo yeyote hasa ya kiteknolojia usalama ni jambo muhimu sana kwa watumiaji wake ndio maana Whatsapp wamezingatia hilo kwa kuto kuwezesha kumfanya mtu mwingine kuingilia mazungumzo au ujumbe unao utuma yaani (end to end encryption).

Kama ilivyo ada kwa ujumbe mwingine wa WhatsApp Status wa video na picha pia kwa ujumbe huu wa sauti utaweza kuchagua watu ambao wataruhusiwa kuusikia (share with) au kuwaangua wale ambao hawataruhusiwa (share with, Except…).
Ukiwa kama msomaji wa makala hii na mmoja wa watumiaji wa WhatsApp umeyapokeaje mabadiliko haya yatakayo kuwezesha kutuma ujumbe wa sauti kwenye sehemu ya Status yako ya WhatsApp. Shuka kwenye uwanja wa kuandika ujumbe,halafu tuandikie kuhusu hili jipya kutoka kwenye mtandao maarufu na wenye watumiaji wengi duniani.
No Comment! Be the first one.