
Ni ukweli uliowazi kuwa hatupo mbali kufanya simu zetu kuwa mbali nasi na isiwe shida kama suala ni kuitumia kwa ajili ya kufanya mawasiliano kupitia WhatsApp.
Mojawapo ya vitu ambavyo nilikuwa nawaza vije kutokea ni uwezo wa mtu kufanya mazungumzo ya WhatsApp kwa njia ya picha jongefu (mnato) kupitia kompyuta. Kitu hicho sasa kinawezekana! Haikuwa rahisi mimi kukubali kuwa siku hizi watumiaji wa WhatsApp Deskop wanaweza kupiga simu kwa njia ya video.
Siku moja nilimpigia simu rafiki yangu kwa njia ya video kupitia WhatsApp na kwa jinsi ambavyo sura yake ilivyowezekana ikanilazima nimuulize siri. Akanieleza kuwa hivi sasa hata kwa kutumia kompyuta mtu anaweza akafanya video call kwenye WhatsApp Desktop.
WhatsApp Desktop yaboreshwa kwa kuongezwa kipengele kitufe cha kuweza kupiga simu kwa njia ya video.
Jinsi ya kuruhusu kipengele hiki kwenye kompyuta ni kama vile tuu ambavyo huwa tunafanya kwenye simu janja ikiwa ni mara ya kwanza kupiga simu katika mtindo huo kwa maana ya kwamba utaona ujumbe unatokea kwenye kioo cha simu kikiomba ruhusa ya kutaka kutumia kamera, kipaza sauti.
Kwa uwezo wa kupiga simu kwa njia ya video kwenye WhatsApp Desktop watakuwa hawaoni kama kuna kitu wamekikosa kwa muda fulani iwapo itatokea amesahau simu janja yake lakini akiwa na mbadala wa kupeza kupokea/kujibu jumbe na hata kupiga simu katika mfumo wa sauti ama picha jongefu.
Usisite kufuatilia TekoKona kila uchwao ili kuweza kupata habari mbalimbali zinazohusu sayaansi na teknolojia kutoka sehemu kila pembe ya ulimwengu.
Vyanzo: WaBetaInfo, DotNet Guide