Ni kawaida kwa huduma mbalimbali za Google huwa zinaingiliana kwa namna moja au nyingine, lakini ulishawahi kufukiria kuwa utaweza endesha mikutano katika Google Meet na kisha mkutano huo uwe unaruka ‘live’ youtube?
Kichafanyika hapa ni kwamba wanaondesha mkutano huo kupitia Google Meet ndio watakao amua mkutano huo uruke kupitia katika ukurasa fulani wa Youtube.

Uzuri wa hii ni kwamba hata wale ambao wako nje ya mkutano huo wa kimtandao watakua na uwezo wa kufuatilia kile kinachoendelea.
Kingine kizuri ni kwamba kupitia huduma hii watazamaji watakuwa na uwezo wa kusimamisha kwa muda, kurudisha nyuma, uwezo wa kutazama baadae mkutano huo n.k.
Ili kuwezesha hili (Google Meet kuruka Youtube) inabidi admin aruhusu jambo hili kuweza fanyika na zoezi hili mpaka liwezekane inaweza kufikia hata masaa 24.

Huduma hii kwa harakla haraka itakuwa iapatikana kwa watumiaji wa Google Workspace ambao wanalipia, hapa nawaongelea “Enterprises Starter, Enterprises Standard, Enterprises Plus, Education Plus.
Huduma hii pia haitakuwa ikipatikana katika watumiaji wa Google Workspace Essentials, Business Starter, Business Standard, Business Plus, Enterprises Essential, Education Standard, Education Fundamentals, Frontline, Legacy G Suite Basic n.k
Pengine labda huko mbeleni hii inaweza kubadilika na watu wengi wakawa na uwezo wa kutumia huduma hii — pengine orodha inaweza ikaongezeka — ni jambo la kusubiria tuu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment. Je utaweza ukawa unatumia huduma hii kwa namna moja au nyingine.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.