fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple IPad IPhone Kompyuta Mac simu

Vilivyotangazwa na Apple katika Tukio la April 2021. #iMac #AirTag #M1

Vilivyotangazwa na Apple katika Tukio la April 2021. #iMac #AirTag #M1
Spread the love

Hivi ndivyo vilivyotangazwa na Apple katika tukio lao la jana. Apple wametambulisha toleo lingine la iPhone 12 – lenye rangi la urujuani (purple) na vifaa vingine kadhaa vipya vinavyotumia prosesa ya kisasa ya M1.

Vilivyotanganzwa na Apple

Vilivyotanganzwa na Apple Aprili 2021

 

Prosesa ya M1 inaleta maboresho makubwa katika vifaa vya familia ya Apple.

1. iPhone 12 ya Urujuani

Toleo la simu ya iPhone 12 yenye rangi ya urujuani litaanza kupatikana rasmi kuanzia tarehe 12 Aprili.

iPhone 12

2. Toleo jipya la iMac / iMac 2021

Apple wametambulisha matoleo mapya ya kompyuta zao za mezani, iMac. Kutokana na utumiaji wa prosesa yao mpya ya M1 kompyuta hizi kwa sasa zitakuwa nyembamba zaidi na nyepesi kutokana na upunguaji wa uhitaji wa feni kubwa na nafasi ya ‘motherboard’ kuwa ndogo kutokana na ubora wa prosesa ya M1.

iMac 2021 vilivyotangazwa na Apple

iMac 2021

Zamani kompyuta hizi zilikuwa zinatumia prosesa kutoka Intel.

SOMA PIA  Microsoft wanataka kompyuta ziwe na sehemu ya laini ya simu

iMac zinakuja na jumba la alumini. Kutakuwa na za rangi mbalimbali; nyekundu, blu, urujuani, njano, silva, na kijani. Kuna maboresho makubwa pia kwenye kamera na spika zake.

  • Resolution ya 4.5K
  • Ukubwa wa inchi 24
  • Kamera ya kiwango cha kurekodi video za 1080p FHD.
  • Kitufe cha Touch ID kwenye keyboard ili kukusaidia kufungua kompyuta kwa haraka

Bei ya chini zinaanzia kwa dola 1,299, na zitaanza kuuzwa katikati ya mwezi Mei.

3. iPad Pro inayotumia prosesa ya M1

Ugonjwa wa Covid-19 umesababisha ukuaji mkubwa wa uhitaji wa tableti na hii ikiwa ni pamoja na za iPad. Katika kipindi cha robo ya mwisho ya mwaka jana, 2020, Apple waliuza iPad za thamani ya dola bilioni 8.44 – ukuaji wa asilimia 41 ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka 2019.

iPad Pro 2021

iPad Pro 2021

iPad mpya nayo inakuja ikiwa inatumia prosesa ya M1, faida nyingine kubwa kutokana na jambo hili ni pamoja na kuifanya iwe kasi kwenye baadhi ya kazi kwa mara 1500 zaidi ukilinganisha na matoleo ya nyuma. Pia utumiaji wa M1 unaifanya iPad Pro kuweza kukaa na chaji kwa muda mrefu zaidi; masaa 10 kwa matoleo yenye WiFi tuu, na masaa 9 kwa matoleo yenye laini pamoja na WiFi. Kingine ni pamoja na uwezo mkubwa wa iPad Pro kuunganishwa na ‘monitor’ zingine na hivyo kukuwezesha kuiunganisha na TV na vifaa vingine kama hivyo.

  • Matoleo mawili: La inchi 11 na la inchi 12.9
  • Kutakuwa na ya RAM na Ujazo tofauti ila kubwa zaidi kwa matoleo yote litakuwa toleo la RAM ya GB 16 na Diski ujazo wa TB 2
  • USB-C
SOMA PIA  Je iPhone 6 plus Yako Inatoa Picha Mbaya? Apple Waleta Programu Ya iSight Kwa Ajili Yako!

4. AirTag

Kupitia teknolojia ya utafutaji wa simu, tablet au kompyuta ya mac ya Find my Device, Apple wameitumia teknolojia hiyo kwa kutengeneza kifaa kidogo ambacho kwa sasa utaweza kukiunganisha na kitu chako kingine chochote ili usihangaike pale utakapokitafuta. Kidude hichi ni kama vile kishikio funguo (Key Holder) na utaweza kukifunga na kitu kingine chochote ambacho unataka kukipata kiurahisi pale utakapokuwa hukioni. Hichi kinaweza kutumika vizuri funguo za magari au nyumba, au ata mabegi yetu muhimu.

AirTag moja itagharimu takribani Tsh 65,000 – Tsh 70,000

 

SOMA PIA  Kipengele Hiki Kinaweza Okoa Maisha Ya Betri Ya iPhone! #iOS13

AirTag moja itauzwa kwa Dola 29 ila nne zitauzwa kwa dola 99. Airtag zitaanza kupatikana mwisho wa mwezi huu.

5. Apple TV 4K

Kumbuka Apple pia wana huduma yao ya kustream filamu na muziki, kupitia Apple TV 4K utaweza kuzipata apps za Apple na ata zile za wengine kama Netflix.

apple 4k tv vilivyotangazwa na Apple

Apple 4K TV

 

Hivyo ndio vitu 5 vikuu vilivyotangazwa na Apple kupitia tukio lao la Aprili.

Apple podcast

App ya Podcast kupata sura mpya

Nje ya hapo kuna huduma zingine mbalimbali ambazo pia zimeboreshwa, hii ikiwa ni pamoja na ujio wa toleo jipya la app ya Podcast – pamoja na huduma ya malipo kwa ajili ya wasikilizaji wa Podcast.

Je una mtazamo gani juu ya maboresho haya kutoka Apple? Tuambie kwenye comment.

Chanzo: Apple

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania